• Facebook
  • Twitter
  • Google Plus
  • Contact

FILM TANZANIA

FILM TANZANIA

  • Home
  • INTERVIEW
  • SIMULIZI
  • HABARI
  • BEHIND THE SCENES
  • LOCATION
  • ABOUT
    • Facebook
    • Twitter
    • Google Plus
Home » SIMULIZI » SAMAKI MTU(MERMAID) 11

SAMAKI MTU(MERMAID) 11

Add Comment
SIMULIZI

 

                                                             SAMAKI MTU(MERMAID)


                                                      SEHEMU YA KUMI NA MOJA


 Simulizi :      SAMAKI MTU(MERMAID) 
 Mtunzi :         Jackson James .
Mawasiliano; +255 762 892 472:, +255 652 064 958
Email: jamesjacson0@gmail.com       


 Gibson akiwa amekaa nyumbani kwao huku akionekana mwenye wasiwasi mwingi kutokana na kazi aliyokuwa ameitoa kwa vijana wake watatu kwenda kukamilisha kazi aliyokuwa amewaagiza ambayo ni kazi ya kumteka Anna na kumpeleka sehemu ambayo aliwaelekeza kwamba watamkuta hapo,Nia na madhumuni ya kufanya kitendo hiki cha ajabu ambacho hajawahi kukifanya kabla ,ni kutokana na na mapenzi ya dhati aliyonayo kwa binti huyo na hakutaka msichana Huyo aweze kuolewa na mtu mwingine yoyote zaidi yake na ninajambo amambalo alimuhaidi Anna siku walipokuwa katika mkesha wa Tamasha la michezo chuoni kwao japo suala hilo Anna alilichukulia kama masihala na kulipuuzia. Baada dakika kadhaa simu yake ya mkononi iliita na alipoipokea alitaarifiwa kwamba tayari zoezi hilo limeshakamilika ,na tayari walikwisha fika katika eneo hilo walilokubaliana kukutana.Gibson alitoka nje ya nyumba yao haraka haraka na kisha alielekea kwenye eneo la kupaki magari yao ,Ambapo aliamua kutumia gari anayopenda kuitumia baba yake ambae ni mfanyabiashara maarufu wa madini ,pindi anapokuwa akienda katika safari zake za mbali,hii ni gari aina ya land cluser,aliingia ya gari hiyo na kuiondoa kwa kasi ili kuwahi katika la tukio waliko vijana wake tayari.Hakuaga nyumbani kwao kwa mtu yoyote kwani hakutaka wajue jambo hilo la hatari linaloendelea katika muda huo,hasa kwa baba yake ambaye ndie alimpa taarifa ya kuhudhuria kwenye hafla hiyo kwani na yeye alikuwa ni mmoja ya wageni walioalikwa na mpaka sasa alikuwa tayari yupo katika sehemu hiyo panapofanyikia Hiyo. Baada ya dakika zipatazo ishirini gari hiyo ilifunga breki pembeni ya ukumbi mkubwa wa sinema ambao kwa muda huo ulikuwa umefungwa na hakukuwa na watu wengi katika eneo hilo kwani ukumbi huo ulikuwa umejitenga mbali na makazi ya watu na ulitumika wakati wa usiku pekee.baada ya kuangakia usalama wa eneo hilo kwamba unaridhisha katika kiasi chake chake ,Gibson alishuka kwenye gari yake nakupiga hatua za haraka kwenda kulifata gari walilokuwemo vijana wake pamoja na mateka wawili ambao ni Anna na dereva aliyekuwa ametumwa kumfuata Anna. 2 Alipokwisha ingia ndani ya gari hiyo alimuangalia Anna kisa akatabasamu ,na kujisemea maneno ya kujiliwaza moyoni kwani hakuwahi kupata nafasi ya kugusa japo hata mkoni wa Anna ambae kwa muda huo alikuwa Yuko kwenye usingizi mzito kutokana na dawa aliyokuwa ameivuta kutoka kwenye kitambaa walichokuwa wamembania pua lake na mdomo. “boss the time is over,its dangerous for us to stay here what are you planning to do with them?”(Mkuu muda umeisha na ni hatari kuendelea kuwa hapa,nini unapanga kufanya nao hawa”,),aliuliza mmoja wa vijana wa gibson huku akiwa waoneshea kidole mateka hao. “just leave them be and let us go”,(waacheni kama walivyo na tuondoke),alijibu Gibson huku akichezea chezea nywele za Anna ,jibu ambalo liliwashangaza vijana wake pia. Vijana Walitii walichoagizwa na Mkuu wao na walianza kushuka kwenye gari mmoja mmoja ,kisha Gibson nae alifata na kujiunga nao kwenye gari aliyokuja nayo na kisha kuondoka kwa kasi, huku wakiitelekeza gari iliyo na mateka hao sehemu hiyo. *************** ********** Katika hospitali kubwa ya NewYork-Presbyterian Hospital,ambayo ni hospitali kubwa na maarufu katika jiji la new York,ndipo walipokuwa wamelazwa mateka wawili waliokutwa ndani ya gari waliloachwa ndani yake na watekaji ambao kwa kipindi hiki bado walikuwa hawajajulikana ni akina nani na walikuwa na lengo gani la wao kufanya hivyo. Baada ya dakika kadhaa baada ya kupigiwa simu ya kutaarifiwa kwamba binti yake ame lazwa kaika hospitali hiyo, Mr john na make wake wakiwa wameambatana na wazazi wa James ,pamoja na james mwenyewe,walifika katika hospitali hiyo kwaajili ya kumuona Anna na dereva wa mr john ,wote wakiwa katika hospitali hiyo kwaajili ya matibabu.Aliyekuwa wa kwanza kuingia ndani ya chumba alicholazwa Anna ni James ,ambae alikuwa na haraka pamoja na wasiwasi mwingi,akitaka kujua hali ya mpenzi wake. “Anna uko sawa,wapi umeumia ?nani aliyekufanyia hivyo? ,mbona hukuniambia?”,aliuliza james ,maswali ya haraka haraka na yanayofuatana ,baada ya kuingia katika chumba alichomo Anna na kumsogelea karibu. “umekuja kuniona? ,Mimi naendelea vizuri sasa ,haina haja ya kuwa na wasiwasi”,alijibu Anna kwa utulivu huku akiunyosha vizuri mkono wake uliokuwa umetumika katika kumtundikia dripu ya maji . “Aaha lakini ni nani aliyefanya hivi?”,aliuliza James ,huku akigeuka nyuma kuwaangalia wazazi wake pamoja na wazazi wa Anna wakiwa wanaingia katika chumba hicho. “ siwafahamu na wala sijawaona”,Alijibu Anna huku na yeye akigeuza macho yake na kuwaangalia wazazi wake na wazazi wa james wakiwa wamesimama na kumuangalia kwa huruma Anna. 3 “samahani sana kwa kuwapotezea furaha yenu ,pia kuwaharibia hafla yenu mliyokuwa mmeiandaa kwa gharama kubwa “,Aliongea Anna kwa huzuni huku machozi yakianza kumtiririka kwanI ni kweli tukio lile lilipoteza furaha na amani aliyokuwa nayo kabla.. “usijali mwanangu cha muhimu ni uhai wako ,haya mengine yatakuja yenyewe ,hivyo haina haja ya kuomba msamaha katika hilo”,alijibu mr John huku akimuangalia kwa macho ya huruma Anna na aliumia sana akipomuona binti yake akilis kwaajili ya tukio hilo ambalo hata yeye hakujua kama litatokea. “Anna acha kulia na kujilaumu bure mwanangu,utakuwa sawa tu “,aliongezea pia Mama yake na Anna huku akishindwa vumilia na kumfuta mwanae machozi yaliyokuwa yakimtoka kama maji. Hali ile iliwafanya wazazi wa james kuwaag wazazi wa Anna ili wao wakakamilishe mambo yakiyokuwa yamebaki katika siku hiyo ikiwemo na la kutangaza kuhairishwa kwa shughuli nzima iliyokuwa imepangwa kufanyika katika Siku hiyo ,kutokana na tatizo lililomkumba mmoja wa wahusika wakubwa wa hafla hiyo ambae ni Anna.james alibaki pamoja na wazazi wa Anna ambao na wao baada ya muda waliondoka na kuhaidi kurejea baadae huku wakimuacha James akiendelea kumuangalia mpenzi wake huyo ambae alimpenda sana na ni msichana pekee aliyekuwa moyoni mwake tangu utotoni. ************** *********** Millian alikuwa amekaa huku akiwa ameinyosha miguu yake kitandani kwake akipokuwa amekaa huku pembeni yake akiwepo baba na mama yake waliokuwa wakiendelea kumpa Huduma mbalimbali na kumfariji binti yao huyo .Ni siku kadhaa sasa zilikuwa zimepita tangu Millian amwambie baba yake wazi kwamba james hakuwa mtu aliyesababisha yeye kupata ajali na wala hana nafasi kabisa moyoni mwake kama baba yake anavyofikiria ,lakini jibu hili halikutoka moyoni mwa millan japo alimjibu vile mr Richard ili kumuepusha James na hasira za baba yake ambazo huweza kumpelekea kufanya jambo lolote kwa mtu yoyote yule bila kujali umuhimu wa mtu huyo kwa mtu mwingine.Ni kweli kwamba Binti huyu aliumizwa sana na kitendo cha baba yake kumwambia kwamba tangu apate ajali na kupoteza fahamu hakuwahi kumuona James akija kumuangalia hata siku moja ili kujua hali yake. Millian alishusha pumzi kwa nguvu alipokuwa akiwaza hayo na kuwafanya wazazi wake kuangaliana na kisha kumuangalia kwa pamoja wakishangaa kitendo cha mtoto wao kuendelea kuwaza na kuwa na majonzi muda mwingi.Millian alichukua simu yake na kuanza kupitia habari mbalimbali mtandaoni ,lakini mapigo ya moyo wake yalienda mbio alipokutana na habari iliyokuwa ikielezea juu ya kuhairishwa kwa hafla ya kuvishana Pete za uchumba kwa watoto wa matajiri wawili ambao pamoja tangu utotoni,na walipendana sana.Taarifa ilieleza kuwa chanzo cha kuhairishwa kwa tukio hilo kubwa ambalo lilitarajiwa kuambatana na kutangazwa kwa mrithi wa kampuni maarufu jijjni new York,ni tukio la kushindwa kufika kwa mmoja wa wapenzi hao kutokana na sababu ambazo hazikuwekwa wazi.Millian alivyozidi kuangalia zaidi alikutana na 4 picha ya james na picha ya Anna,wakitajwa kama wapenzi waliotarajiwa kuvishana Pete za uchumba siku .Millian alishindwa kuvumilia mshituko mkubwa alioupata baada ya kuona picha hizo na alijikuta akiishiwa nguvu mwilini na kupoteza tena fahamu,mbele ya macho ya wazazi wake. •

0 Response to "SAMAKI MTU(MERMAID) 11"

← Newer Post Older Post → Home
Subscribe to: Post Comments (Atom)

FOLLOW US

POPULAR POSTS

  • KILA MWANDISHI WA MISWADA {SCRIPT}
    Kila mwandishi wa miswada {script} hutumia njia aipendayo kuitumia katika kuandika miswada {script}si kwa nchi yetu ya Tanzania pekee h...
  • IFAHAM HISTORIA YA KANUMBA YOTE KWA UJUMLA
    Hayati Steven Kanumba amezaliwa Januari 8 ,1984 Shinyanga,Tanzania Amefarki Aprili 7, 2012 (umri 28)Dar es Salaam,Tanzania Kaz...
  • SAMAKI MTU(MERMAID) 01
                                                                                                             SAMAKI MTU(MERMAID)   ...
  • MZEE MSISIRI ATUMBUA JIPU
    •••• ♦ •••• ♦ •••• ♦ •••• ♠ ••• ♦ 1. Jina langu kamili ni FADHILI RAJABU MSISILI 2. Kabira langu ni Chotara wa kizigua kwa baba na ...
  • SAMAKI MTU(MERMAID) 04
                                                                                                                          SAMAKI MTU(MERMAID...
  • ULINGO WA MOTO FILAM YA MAPIGANO YENYE UARISIA
    Daaah!!! Nikali tena ni noma sana,Usisa hau wala usikose kupata nakala yako.Tarehe 23/4/2018 filamu hii itakua tayari imo sokoni.....UL...
  • SAMAKI MTU(MERMAID) 02
                                                           SAMAKI MTU(MERMAID)                                                        ...
  • MFAHAM JUMA KILOWEKO SAJUKI
    Sajuki alizaliwa mwaka 1984, mkoani Songea na kupata elimu yake ya msing na sekondari hukohuko mkoani Songea.Ambapo mwaka 2005 aliweza ku...
  • JINSI YA KUTENGENEZA FILAM NA KUUZA
     KATIKA miongo kadhaa iliyopita filam nyingi zenye mafanikio zimetokezwa huko Hollywood. Hilo limekuwa na uvutano mkubwa ulimwenguni pote ...
  • SAMAKI MTU(MERMAID) 11
                                                                   SAMAKI MTU(MERMAID)                                                 ...
Back to top!
Copyright (c) 2014 FILM TANZANIA. All Rights Reserved Created by Flash TZ Blog. Designed by Flash TZ Blog. Powered by Blogger.