Hayati Steven Kanumba amezaliwa
Januari 8 ,1984 Shinyanga,Tanzania
Amefarki Aprili 7, 2012 (umri 28)Dar es Salaam,Tanzania
Kazi yake Muigizaji,Mtunzi,Mtayarishaji,Muongozaji
Steven Charles Kanumba (8 Januari1984,Shinyanga-7 Aprili2012) alikuwa msanii wa maigizo na filamu kutoka nchini Tanzania. Katika historia ya tasnia ya filamu nchini Tanzania, Kanumba ndiye aliyekuwa msanii wa kwanza nchini kufanya kazi nje ya nchi na kuweza kuwavuta wageni kutoka nchi mbalimbali kuja kuigiza Tanzania. Hasa walikuwa Wanigeria kama vile Mercy Johnson, Emmanuel France, Nkiru Silvanus, Ramsey Nouah, na wengine wengi tu. Kanumba pia ameweza kuwaleta waongozaji filamu kadhaa was Kinigeria nchini.
Maisha
Steven alianza masomo yake katikashuleya msingi yaBugoyi, na kuendela na masomo ya sekondari huko Mwadui na baadae kupata uhamisho katika shule moja jijini Dar es Salaam iitwayo Dar Christian Seminary. Alivyomaliza kidato cha nne akaendelea na masomo ya kidato cha tano na sita katika shule ya sekondari ya Jitegemee ilioko huko huko Dar es salaam.
Kanumba ameanza shughuli za kuigiza miaka mingi kwenye miaka ya “90”. Ila kufahamika zaidi alianza mwaka2002 mara tu baada ya kujiunga na kundi la sanaa ya maigizo maarufu kama Kaole Sanaa Group.
Steven Kanumba hivi sasa amejibebea umaarufu mkubwa nchini Tanzaniana amekuwa kipenzi cha wengi na amekubalika karibuni nchi zote zaAfrika Masharikina maziwa makuu.
Kwa sasa ameanza kutangaza sanaa nchi za Afrika ya Magharibi ikiwemo Nigeriana pia Wanigeria wamependezewa na uigizaji wake hivyo kushirikiana pamoja naye katika filamu kadha wa kadha. Filamu ambazo wameshawahi kushirikiana pamoja ikiwemo na ile yaDar to Lagos,She is My Sisterna nyingine ambazo bado zinajengwa.
Baadhi ya filamu na Tamthilia Alizoshiki
1Tufani( Johari )
2Gharika
3Baragumu
4Sikitiko Langu
5Johari 2
6Dangerous Desire
7Dar 2 Lagosi
8Cross my Sin
9Village Pastor
10Family Tears
↑Rudi Sehemu A
Filamu na Tamthilia Alizoigiza
1Jahazi( Tamthilia )
2Dira( Tamthilia )
3Tufani( Johari )
4Gharika( Tamthilia )
5Baragumu( Tamthilia )
6Sikitiko Langu(Filamu)
7Johari 2(Filamu)
8Dangerous Desire(Filamu)
9Dar 2 Lagosi
10Riziki (film)(Filamu)
11Cross my Sin(Filamu)
BONYEZA HIYO PICHA