Kila mwandishi wa miswada {script} hutumia njia aipendayo kuitumia katika kuandika miswada {script}si kwa nchi yetu ya Tanzania pekee hata nchi za wenzetu, kwa kukuaminisha nimeamua kukuwekea picha tofauti tofauti. Endelea kufuatilia habari hii iliyopana zaidi usikate tamaa punguza uvivu ili upate elimu japo kwa uchache na kiupana zaidi.
THREE ACT STRUCTURE [VITENDO VITATU VYA MUUNDO]
Muundo unakuwa na mlolongo wa matukio unawekwa au kupangwa katika makundi makuu matatu kwa jinsi yanavyotokea katika story muundo huu ndio utampelekea mwandishi kuufuata anapoandika story au script.
Setup [kuanzisha ]confrontation [mapambano] na resolution [azimio] lakini wengine hutumia beginning [mwanzo] middle[katikati] na end [mwisho]
ACT ONE: SETUP /BEGINNING
Huu ni mwanzo wa filamu hapa wahusika itabidi kutambulika ajulikane nyota, adui na msaidizi au wasaidizi wa nyota pia ifahamike mahusiano yao yamkini wao kwa wao au kwa jamii kazi na mchango wao,wapo katika ulimwengu gani ulimwengu utoe picha kamili sio wasaidizi wa nyota aonekane mwanzo.
ACT TWO: CONFROTATION /MIDDLE
Muhusika anaamua kulikabili tatizo au anapata msaidizi [wasaidizi ]wakumsaidia kukabili matatizo aliyonayo ni vizuri visa viwe vya ubunifu wa kutosha muhusika mkuu asilifikie hitaji lake kirahisi.
ACT THREE: RESOLUTION /END
Maswali yaliyozaliwa mwanzo wa filamu yanatakiwa kujibiwa hapa muhusika mkuu baada ya kupata mitihani na kuyatatua anastahili ashinde huku mwisho ndiko kuna somo la kujifunza kwa watazamaji pia hakuna utazima. Mwisho muhusika kushinda inategemea dhumuni la story iliyoandikwa.
MISINGI YA KUZINGATIA KATIKA UHANDISI WA MUSWADA [SCRIPT]
Unapoandika mswada [script] kuna vitu vitatu vya msingi unavyotakiwa kuzingatiwa, muhusika [character] muundo [plot] na dhamira [theme].
Script ya filamu inayo sehemu kuu nne ambazo kila mwandisi lazima azipitie ili scriptyake iwe nzuri, kwanza kabisa awe na hadithi [story] wazo [idea] kamili hatua [stage] kuzizingatia.
MUUNDO:
Ni suala la msingi kuzingatia muundo wa hadithi ndio inayoonekana matukio na nini kinachotokea katika hadithi hiyo,mtindo wa maneno na vitendo vilivyopangwa vizuri na kuongeza matukio katika hadithi.Muundo umegawanyika katika sehemu kuu tatu yaani mwanzo, kati na mwisho huwa inatege
mea na mwandishi mwenyewe waandishi wengine huanza mwisho kwenda mwanzo au muundo wa moja kwa moja vile vile matendo yanaweza kuelezea story kama inavyokuwa katika riwaya mara zote unapoandika hadidhi lazima uanze na swali na kila filamu huwa inayo furah una udhuru.
DHAMIRA:-
Kabla ya kuandika story lazima ujiulize maswali na ujibu, majibu yako yakusaidie upangilie mtiririko mzuri wenye kuvutia kwa kila atakye soma hadidhi au atakaye tizama filamu yako maswali ya kujiuliza ni hayo yafuatayo:-
Muhusika mkuu ni yupi?
Anapata vizuizi gani?
Kitatokea nini endapo atashindwa kufikiria malengo?
Scene inaanzia wapi na inaishia wapi?
Je kuna uhusiano wowote kati ya tukiol (scene) moja na nyingine?
Je ,atukio yako yanapooza (flat) na kujirudia rudia kutikuwa na mvuto?
Je mtazamaji atafurahia kuangalia filamu yako?
Hayo ni maswali ya kujiuliza na ya msingi kwa kila mwandishi akiyazingatia mwisho wa siku ataandika mswada mzuri na kila mtu ataupenda. Ubunifu ni muhimu kwa kila mwandishi na ubunifu huo unapaswa uendane na mlolongo wa hadidhi yako pia jambo la msingi katika script mgongano (conlict) mgogoro.
Lazima kuandika kwa kuonesha eneo kama nje au ndani alafu ni sehemu gani sebuleni, chumbani kwa kufuatiwa muda kama mchyana au usiku ni lazima iandikwwe kwa herufi kubwa, usiandike aina ya shots zitakazotumika ili muuongozaji (director) aweze kuweka mawazo yake au ujuzi wake inaweza kuwa shots ulizoziandika yee hazimvutii.
CHARACTER:-
Wahusika wanayoifanya story ikamilike kwa kuitumia script kama muuongozo wao na kujijua wanachokifanya, pasipo wahusika katika filamu, kuna mambo mengi yanayowahusu wahusika ili kuifanya story iwe ya kusisismua na yenye mvutao.
Wahusika wanao mchango mkubwa sana iwapo mwandishi ataweka umakini kwa wahusika pindi atakapoandika story. Muhusika awe anabadilika au kusogea mbele pamoja na story lakini anapoandika ndipo na story hubadilika. Katika uandishi wa script ni muhimu kuwa na majina ya sanaa ili kuleta mvuto, hii ni sanaa uwanja wa uchunguzi wa majina ni mpana sana lakini muhimu kumpatia jina au cheo kutokanana na muonekano wake pia usimpatie jina gumu ili iwe wepesi kwa watazaji, baadhi ya eazamaji hupenda kuchukulia mifano kutokana na muhusika kuitendea haki story.
Uandishi wa script nimchanganyiko wa sayansi na sanaa kwa pamoja, unadishi wa script huitaji mtu mbunifu na mwenye uwezo wa kuchanganya ladha mbalimbali kwa lendo la kutoa kitakacholeta mtazamo mpya kwa jamii anayotaka kuigusa. Mwandishi wa scipt katika endo hili ni mkemia wa fasihi mwenye uwezo kubadilisha maandishi kasha kufanya maandishi yaonekane kama viumbe ndani ya karatasi kupitia muigizaji kwa kufuatilia nguzo kuu za kutengeneza filamu ambazo ni kipande kikuu cha uigizaje (master scenes), uigizaj kwa matendo (Action) na mazungumzo (dialogue).
Uandishi wa script ni sanaa yenye kutumia ubunifu mkubwa na suala kubwa la kubuni kamwe si jepesi kila wakati unapoangalia vipindi vya luninga au filamu hata kucheza mchezo unaotumia kumpyupa (game) vyote vimeandikwa kwanza na binadamu.
Lep soko kubwa la sanaa linahitaji ubunifu ili kuleta ujumbe utakaofanikiwa kwa ufasaha, hata hivyo uandishi wa script unaweza ukawa mgumu na wenye kushosha kutotokana na ugumu, mwandhishi anaweza kujikuta baada ya kumaliza kuandika script ya filamu moja akakaa mwaka mzima bila kuandika tena.
Swali:-
Kiama unaanza kuigiza katika uandishi wa script za filamu na maigizo hje umejidhatiti namana gani ili kuendelea mbele?
Tambua:-
Script iliyoandikwa vizuri inasomeka haraka kuliko script ambayo haijaandikwa vizuri, ilivyoandikiwa vizuri unaweza kusoma ukurasa wa kwanza hadi wa mwisho kwa mtiririko, mawazo yatakufanya kama unaangalia picha wakati wa kusoma script unaweza usikwame hata ukurasa mmoja ukijaribu kutafakari ni kitu gani kitatokea ni njia iliyobora ya kutengeneza adhira kwa msomaji kwa kuionesha na sio kusimulia wala usiongeze kusimulia ni kitendo cha mtu kuelezea jambe ambalo linaweza kuonekana kama script yako inazungumzia jambo lililopita bora tulione katika kumbukumbu au mawazo (flashback), kiama unazumgumzia muhusika anafanya jambo Fulani ni bora aonekane akifanya jambo kuliko kutoonesha hilo tendo. Mfano:- Muhusika akimwambia mpenzi wake anampenda itapendeza tukiona anampa maua akionesha ishara yoyote itakayoonisha kama muhusika anampenda mpenzi wake, muhusika kama amekwazwa ni vizuri zaidi tuone kitendo kilicho mkwaza.
Script yako ili isipunguze kasi ya usomkaji usijaribu kuweka shots, sehemu gani kamera (camera) iwekwe, jinsi wahusika watakavyo zungumza n.k.
IDEA (WAZO)
Zipo sababu nyingi za tasnia ya filamu Tanzania haina faida kubwa kulinganisha na nchi zingine zilizoendelea katika masuala ya filamu, ili faida iwe nzuri ni lazima tuepukane nayo masuala haya yafuatayo nitayataja machache.
Script zilizokosa ubunifu.
(Technology) technologia duni.
(Actors and Actress) waigizaji wasio na kipaji.
Elimu ndogo kwa kila (crew) wafanyakazi
Umasikini wa kifedha katika kuandaa filamu
Utandawazi
Script ya filamu ni moyo wa tasinia ya filamu hii ndiyo inayohamasisha filamu ichezwe namana gani ndiyo inayotoa muongozo kwa wansanii kasha kuonekana katika luning, script ilinzuri ni lazima ipangiliwe mazungumzo na matendo yote kwa ujumla namna ambayo wazo litafsiriwe sawia na kuonekana kupitia luninga sawa na mawazo li kutimiza.
Mwandishi kama unayo (idea) wazo la story basi ainisha kwanza sehemu nzuri za kufanya hiyo idea, mahusiano ya tabia (characters) na wasifu wao, lazima pia ujue ni idea ipi imebeba story nzima na namna hao characters watashirikiana kuikamilisha idea hiyo, idea nzuri sio lazima iwe ambayo haujawhai kuisikia bali ni ile ambayo inasisimua na inatoa nafasi ya matukio mengi ili kuikamilisha.
Usichague idea ambazo hauna umahirinazo mpaka utakapokuwa tayari kujifunza na kufanya utafiti (research) juu ya mambo yanayohusu hiyo idea.
(Dialogue) mzungumzo ya kwenye script kwa kawaida zinatofautina na ziwe za ubunifu, maana dialogue za kwenye script zinakua na uhai zenye (speed) kasi ya kutimiza lengo Fulani wakati hazina haraka kwa kuwa muda haunani, wala budget, wala hazikaririwi. Usiwe na haraka ya uandishi jipe muda wa kufikiria na kuyapangilia mawazo katika mtiririko utakaoeleweka kutimiza script, ni vizuri story uigawe katika vipengele vitatu:-
Utangulizi - hapa unawatambulisha wahusika na mahusiano yao, wasifu na
chanzo cha kisa.
Mgogoro - kisa kimetokea na namna gani kinavyoadhiri wahusika au
muhusika.
Hitimisho - kisa kimeleta madhara, utatuzi unafanyika ndipo linapatikane jibu
la kile swali wa mwanzo wa hiyo story.