SAMAKI MTU(MERMAID)
SEHEMU YA KWANZA
Simulizi : SAMAKI MTU(MERMAID)
Mtunzi : Jackson James .
Mawasiliano; +255 762 892 472:, +255 652 064 958
Email: jamesjacson0@gmail.com
Ni asubuhi tulivu jua likichomoza taratibu, mawimbi ya bahari ya pacifiki yakiwa yanaenda kwa kasi ndogo ,kabisa kuashiria utulivu wa bahari kwa siku hii ya Leo.samaki wengi wakubwa kwa wadogo walionekana kuogelea na kuruka ruka huku na huko wakifurahia mwanga mdogo wa jua uliopenya na kuingia chini ya bahari,pamoja na maji ya chumvi ambayo wameyazoea katika maisha yao ya kila siku,katika jiwe moja kubwa liliko chini ya bahari hii anaonekana samaki mmoja ambaye kimwonekano anaonekana tofauti na samaki wengine kwa sababu alikuwa na umbo la ajabu kiasi cha kufanya samaki wengine kumuogopa na kukimbia kila alipokuwa akionekana mbele ya macho yao.hii ni kwa i samaki huyu alikuwa na umbo la binadamu wa kike kutoka juu hadi kiunoni lakini alikuwa na umbo la samaki kutoka kiunoni hadi miguuni hii ndo tofauti kubwa iliyoonekana kati ya samaki mtu huyu aliyekuwa mrembo na wakuvutia kisura, na samaki .Alikaa kwa muda pale kwenye jiwe huku akifikiria mambo yaliyotokea wiki moja iliyopita katika bahari hiyo ya pasifiki hasa machafuko makubwa ya bahari (sunami) yaliyosababisha maafa kwa samaki wengi na ndugu zake pia ambao walikuwa ni sawa na familia yake wote walipoteza maisha na kumuacha yeye akiwa mpweke na asijue nini cha kufanya kwa wakati huo kutokana na kwamba ndo samaki pekee wa aina yake aliyebaki katika bahari hiyo ,jambo hili ndo lilimfanya ajihisi mpweke na kubaki na mawazo huku akilaumu aliyemuumba katika hali hiyo lakini hakukua na majibu yoyote kutoka kwa huyo aliyeamini kwamba ndo amemuumba hii ilimfanya apige mbizi taratibu na kurudi chini ya pango kubwa lilipo chini ya bahari hii yalipo makao yake.
Katika kisiwa cha mariana nchini marekani, Pembeni mwa kidogo mwa bahari panaonekana jumba kubwa na la kifahari lenye kila sifa ya kuwa jumba lenye mvuto zaidi kuliko majumba mengine yaliyozunguka sehemu hiyo iliyojaa majumba na starehe za kila aina pembeni mwa bahari kubwa ya pasifiki.Nje ya jumba hili panapendeza na kuvutia macho kwa Maua,bustani na mandhari ya kuvutia.kwa haraka wengi walioliona jumba hili walijua ni makazi ya tajiri mashuhuri au kiongozi
2
mkubwa wa serikali lakini ilikuwa ni vigumu kwao kuamini anayeishi katika jumba hili ni MTU mmoja pekee tena akiwa kijana mdogo kabisa.
Ndani ya chumba kimoja katikajumba hilo kuna mlio unasikika…..ngriiii……ngriiii…. …ni simu ya mezani iliyokuwa ikiita pembeni mwa kitanda kikubwa na chenye kila sifa ya kuitwa cha kifahari ,juu yake alikuwepo kijana mmoja ambaye alikuwa ni mzuri wa sura na mtanashati kutokana na mwonekano wa kitanda na chumba alicholala kuwa cha kuvutia macho na kupendeza. huyu aliitwa james ,ambaye ni mtoto wa tajiri mmoja mkubwa katika jiji La newyork Marekani. Alijivuta taratibu na kupeleka mkono kwenye simu huku akionekana kulaumu kimoyo moyo huyu anaempigia simu muda huo wa asubuhi iliyotawaliwa na baridi Kali kiasi cha kumpa usingizi mzuri na uliompa pumziko la uchovu aliokuwa nao kutokana na kusoma kwa muda mrefu kiasi cha kuchelewa kulala,alishika kichwa cha simu mkononi kabla ya kujigeuza huku na huko huku akiambatanisha miayo mikali iliyodhihirisha uchovu aliokuwa kabla ya kuipokea…. “Hallow James its time for class where are you now?” (haloo James ni muda wa darasani ,upo wapi sasa), ilikuwa ni sauti ya msichana mmoja wa kizungu anayesoma darasa moja na James katika chuo kikuu cha oxford university .” hii mllian,am sleeping now but I will come within few minutes”(habari milliani nimelala sasa ,lakini nitakuja baada ya dakika kadhaa),,alijibu james huku akirusha pembeni blanket zito alilokuwa amejifunika siku hiyo.”” Ok fine don’t be late James am on my way now”(sawa James usichelewe Mimi nipo njiani ,sasa”” aliongeza milian.”ok”(sawa) alijibu James kisha simu ikakatika haraka haraka aliweka miguu chini na kuchukua viatu vya kukanyagia na kwenda bafuni kwaajili ya usafi wa mwili. Alitumia muda wa dakika kadhaa katika kufanya usafi wa mwili kabla ya kuandaa vifaa vyake kwaajili ya kuwahi chuo ,alirudishia mlango wa chumba chake vizuri na haraka haraka alishuka ngazi kuelekea sebuleni ambako kulikuwa kumepambwa kwa malumalu za kila kila aina pamoja na samani za gharama kubwa,sebule hii ilikuwa mithili ya ikulu ndogo ya rais wa nchi,upande wa kushoto wa sebule hii juu ukutani palionekana picha mbili kubwa moja ya James,lakini ya pili ilikuwa ni ya watu wawili wakiume na wa kike,wakiwa pamoja na James ,bila shaka hawa ni wazazi wa james yaani baba yake na mama kwa mwonekano wa picha hii inaonyesha James ndo mtoto wa pekee kwa wazazi wake.”nitawaona siku sio nyingi wazazi wangu’alijisemea James moyoni mwake huku akijiandaa kushuka ngazi ya mwisho ili kuifikia sebule ,haraka haraka alichukua funguo ya gari yake na kufunga mlango wa nje ya nyumba kwa nguvu na kupiga hatua za haraka hadi kwenye gari kisha akaiwasha na kuondoka kwa kasi kuelekea chuoni.
Tangu akiwa mdogo James alipenda sana kuwa mchunguzi na mtafiti wa mambo mbalimbali yahusuyo jamii na Yale yaliyowasumbua vichwa watu wengi hasa wataalamu waliopenda kuchunguza mambo yanayosadikiwa kuwepo lakini hayakuweza kuonekana katika upeo wa macho yao.kutokana na kupenda kujifunza na kuuliza bila kukata tamaa ,James alipata mafanikio makubwa katika masomo yake tangu aanze elimu ya awali mpaka sasa chuo kikuu.Lengo kubwa kwake ni kuwa mtaalamu mkubwa na mtafiti mashuhuri katika elimu inayohusu viumbe hai waishio majini.
3
Katika kipindi cha muda mrefu katika visiwa vya mariana Marekani kumekuwa na fununu za kuwepo kwa viumbe wa ajabu waitwao samaki watu (mermaid)ambao wamekuwa wakionekana katika fukwe za bahari ya pasifiki Mara kwa Mara,lakini wengi wao walipatikana wamekufa katika sehemu mbalimbali za fukwe ya bahari hiyo kutokana na tsunami iliyo ikumba bahari hiyo wiki moja iliyopita.Taarifa ya kuonekana kwa viumbe hao wa ajabu ilisambaa kwa kasi sana katika maeneo mengi ulimwenguni na kutikisa vichwa vya wataalamu wengi wa masuala ya viumbe duniani kote,taarifa hii pia ilikuna akili ya James ambaye pia alitamani sana kujua kwa undani kuhusu viumbe hawa wa ajabu kwani ndo taaluma anayoichukua kwa sasa katikà chuo ,lakini lililomuogopesha zaidi na kukaribia kuvunja moyo wake ni kusikia aina hii ya viumbe wamepotea na hawajaonekana kabisa katika kipindi cha wiki moja tofauti na ilivyokuwa mwanzo kabla ya tsunami kukumba kisiwa ,hii ilimfanya James kuona kama itamuwia vigumu kuwa mtafiti mkubwa na wakwanza kujua kwa undani juu ya viumbe hawa,lakini alijipa moyo na kuamini siku moja atatimiza malengo yake.”usijali James hawa viumbe bado wapo hivyo utatimiza kile unachokihitaji” alijisemea James, kabla ya kushtushwa na sauti ya millian iliyomtoa katika ulimwengu wa mawazo ,,,”hey james let us go to class now”(James naomba twende darasani sasa) ,”ooh ok let us go millian”(aah sawa twende millian),alijibu James huk akifunga mlango wa gari vizuri,kisha akachukua vifaa vyake na kuambatana na millian kuelekea darasani.
Kama ungeambiwa kuchagua warembo katika chuo cha oxford university marekani usingeacha kumchagua binti millian mtoto wa tajiri mkubwa na mfanyabiashara maarufu kisiwani Mariana,hii ni kwa sababu ya mvuto alionao binti Huyo kwa wavulana na hata wanaume wa makamu walikuwa wakimtolea macho ya tamaa,kutokana na kujaliwa umbo zuri,sura nzuri na matunzo bora kutoka kwa wazazi wake binti huyu wa kizungu ,alitishia hatima ya ndoa nyingi katika kisiwa kikubwa cha Mariana ,mbali na kupendwa na kuhitajika kwa hali na Mali kwa wanaume wengi wenye fedha,Mali na kila sifa ya kuitwa matajiri bado moyoni kwa binti huyu mdogo mwenye umri wa miaka 22 pekee,alikuwa amemweka kijana wa kiafrika mwenye asili ya kitanzania aitwaye James,tangu aanze kumfahamu kijana huyo imekuwa ni vigumu kutoa nafasi kwa wanaume wengine walio mhitaji yeye kwa kila hali,mbali na kumpenda kwa moyo wa dhati kijana Huyo mtanashati lakini imekuwa ngumu kumuonyesha James kile alichonacho moyoni mwake juu yake,hii inasababishwa na James kuonekana kama MTU asiyejali wasichana wa aina yoyote chuoni na muda mwingi kuonekana yupo bize na masuala ya masomo,hii ilimfanya millian kuwa kama mtumwa wa mapenzi kwa kumfuata fuata James kila mahali japo aweze kuufariji moyo wake japo kwa mbali.Licha ya kuwa binti pekee pamoja na mdogo wake wa kiume aitwaye johonson,katika familia ya Mr Richard mwenye utajiri wa kila aina ,bado hii haikutosha kumfanya binti huyu amsahau James japo Mara moja tu moyoni mwake,ni kweli kwamba alipata kila anachokihitaji kutoka kwa wazazi wake,lakini alikosa hitaji kuu la moyo wake ambae ni kijana James.
Tangu ahamie jiji la newyork miaka 20 iliyopita akitokea Tanzania ,amekuwa ni mtu maarufu sana hasa katika jiji hilo kutokana na umaarufu mkubwa na umilikaji wa kampuni kubwa ya uzalishaji wa saruji na vifaa vingine vya ujenzi,vyote hivi vimemfanya aweze kupiga hatua kubwa kimaendeleo kiasi cha kutangazwa kama tajiri wa 4 katika jiji hilo ,yeye na mke wake mrs david,walikumbana na changamoto nyingi sana ambazo zilihitaji kuwakwamisha katika safari yao ya mafanikio hasa ubaguzi wa rangi ambao katika kipindi cha miaka 16 iliyopita ilikuwa imepamba moto katika
4
maeneo mengi ya marekani,licha ya kuvumilia hayo yote na kuweza kutimiza malengo yao ,ambayo yamewafanya hadi sasa kuwa kati ya matajiri wakubwa na wanaogopeka jijini new york,bado waliona kunauhitaji wa siku moja kukumbuka asili yao ,yaani mahali walipozaliwa ambapo ni Tanzania,tajiri huyu aliamini kwamba kuendelea kumuaminisha kijana wao wa pekee ambaye ni James ,kwamba newyork ndo kwao haitakuwa vyema kwani tangu udogoni wamekuwa wakimfundisha kijana wao lugha ya kiswahili,licha ya kutumia pia kingereza,wazo hili lilimpa mzee huyu uamzi wa kuanza maandalizi ya kumiandalia makao mtoto wao nchini Tanzania Ili anapomaliza na kukamilisha masomo yake aweze kufanya shughuli zake na kuendesha maisha yake huko . huyu anaitwa Mzee David john ,ambaye ndo baba mzazi wa kijana James ,ambaye ni mwanachuo katika chuo cha oxford university marekani..
Ni siku ya tarehe 12/6/2003 ,upepo wa bahari ukipuliza taratibu kuelekea upande wa mashiriki na kuyafanya mawimbi ya bahari ya pasifiki nayo kwenda taratibu kulingana na kasi ya upepo,upande wa chini ya bahari hiyo kubwa karibu na kisiwa cha Mariana ,anaonekana samaki mmoja mwenye umbo la binadamu wa kike upande wake wa kiunoni mpaka kichwani,lakini akiwa na umbile la samaki katika upande wake wa kiunoni hadi miguuni,samaki mtu huyu alipiga mbizi taratibu akifatisha mawimbi ya bahari na mwanga wa jua ulipokuwa unatokea,kwa kweli kwa hali ya kawaida ni ngumu kuamini kama ni samaki unapomuona kwa mbali kutokana na uzuri wa sura na umbile aliloumbwa nalo samaki huyu ,alikuwa na mawazo mengi kichwani akifikiria namna gani atayaanza maisha yake mapya akiwa ndo samaki pekee wa aina yake katika bahari hiyo kubwa kwa sasa,wakati akiwa na mawazo mengi alishtushwa na mwanga wa jua uliomchoma machoni kuashiria amefika nje ya kina cha maji yaani nchi kavu ,alijivuta na kupanda juu ya mwamba tambarale uliokuwa pembeni mwa ufuo wa bahari,sehemu hii hupenda kukaa Mara nyingi anapotoka nje ya bahari nakuja nchi kavu ,hvyo ni sehemu aliyoizoeq kwani ni Mara chache inafikiwa na binadamu wa kawaida ,lakini samaki huyu pindi anapokaa hapa huweza kuwaona binadamu wote wanaokuwa katika ufuo huo wa bahari ,ambao upo katika kisiwa cha Mariana.,Mara zote amekuwa akiwaza namna yeye anavyoonekana tofauti na binadamu wa kawaida ,” kwanini Mimi Niko hivi” aliwaza samaki yuleakipeleka mkono wake kichwani a kugusa nywele zake ndefu ,,kingine kilichomshangaza ni kwamba yeye hana uwezo wa kuongea tofauti na binadamu wa kawaida,alibaki kushangaa tu pindi aliposikia sauti za binadamu kwa mbali wakiwa wanazungumza,””inaonekana Mimi nitofauti na wao kwa kila kitu”,aliwaza akilini kwake huku akirusha rusha miguu yake iliyoungana nakutengeneza umbile la mkia wa samaki,kabla ya kuondolewa katika dimbwi la mawazo baada ya kuona binadamu kadhaa wakiwa wakiwa wanatembea na kusogea upande aliokuwepo,”alijivuta na kujirusha majini na kuanza safari ya kurudi makaoni kwake.