SEHEMU YA KWANZA
Simulizi : URITHI WANGU
Mtunzi : RAJAB JK MWABUSEGA
Mawasiliano; +255 71653 8398
Siku zote katika maisha kuna kupanda na kushuka, pia viyu hivyo huo
haupangi wewe mwenyewe pale unapopata shida au karaha ndani ya maisha yako
ndipo vinatokea vitendo hivyo.
Binadamu tunayo sifa kubwa ambayo ni kurithi na sifa hiyo huwa inatokea
ndani ya familia au katika ukoo, vitu huwa vinarithiwa, akili hurithiwa na kuna
utata mkubwa katika kurithi mali na hakuna kipingamizi pale binadamu
aporithishwa akili na mwenyezi mungu.Sio familia zote akili za wazazi hufanana
na akili za watoto wao, nimeamini hilo kutoka kwa mama yangu mlezi aliye nilea
tangu nilipokuwa kichanga hadi kufika
umri wa kujua baya na zuri.
Kuna mambo mengi aliyonitendea mama yangu mlezi, ila yalikuwa tofauti
pale mnapokuwa nae yeye na ninapokuwa na watoto wake.Kulikuwa kuna siri kubwa
kwa mama yangu mlezi ambayo sikuijua mimi na hata watoto wake hawakuijua, siku
ilipojua siri hiyo niliona mwili wangu mzito.
Kwa kuwa tupo pamoja naomba twende sawasawia ili ujue mambo yaliyotokea
na kisa nini hadi yanitokee mikasa ile, mkishajua itakuwa vizuri kuwafikishia
ujumbe wale wenye tabia kama ya mama yangu mlezi wabadilike.
Japokuwa sikupata bahati ya kuonana na mama yangu mzazi nilipata habari
kwamba nimefanana naye.Baada ya mama yangu kupata umauti, baba alichukua uamuzi
wa kuoa mwanamke mwingine awe mrithi wa mama yangu mzazi ili nipate malezi
yaliyo bora ya baba na mama.
Katika ndoa yao walibahatika kupata watoto wawili mapacha, mmoja wa
kiume na mwingine wa kike.
Watoto hao maisha yao yalikuwa nje ya nchi ya Tanzania kimasomo.Ilikuwa
kila baada ya likizo kubwa huwa wanarudi hapa nchini tanzani, wakiwa hapa huwa
nakuwa na furaha pia upweke hunikimbia.
Mama yangu mlezi aliamua kuwaandikisha katika shule moja maarufu hapa
nchini, ukaribu wetu ulikuwa umezidi kati yangu na wale wadogo zangu cha kushangaza
mama yangu mlezi aliwakataza wasiwe karibu na mimi.Lakini kila atakachowaeleza
nao lazima waje waniulize maswali kuhusu maisha ya pale nyumbani.
Nilipokuwepo chumbani kwangu nimelala, ghafla mlango nilisikia
ukigongwa kwa hasira bila kusikia sauti ya mtu.Nilipofungua mlango nilivutwa
kwa hasira huku nikipigwa makofi usoni mwangu.
“Aliyekutuma uende shule nani?” aliniuliza huku
akinipiga makofi.
“Hajanituma mtu.”
“Nimesema sitaki nikuone umetoka humu ndani..”
“Ndiyo, nimekuelewa.”
“Nikisikia umeenda tena nitakachokufanya utajuta
kuzaliwa..”
“Lakini mama….” alinikatisha kusema
“Lakini nini.? Na mimi si mama yako unasikia wewe
paka..?”
“Mimi pia ni mtoto wako ujue hilo?”
“Sina mtoto kama wewe?”
“Nikufanyie kitu gani ili nipate upendo wako..?”
“Upendo wangu wanaostahili kupata ni watoto wangu tu..
na si
wewe.?” mama
yangu mlezi alinikata maini kwa maneno yake.
“Laiti kama watoto wako wangekuwa wanafanyiwa hivi,
Kama wewe
unavyonifanyia mimi ungejisikiaje..?”