• Facebook
  • Twitter
  • Google Plus
  • Contact

FILM TANZANIA

FILM TANZANIA

  • Home
  • INTERVIEW
  • SIMULIZI
  • HABARI
  • BEHIND THE SCENES
  • LOCATION
  • ABOUT
    • Facebook
    • Twitter
    • Google Plus
Home » SIMULIZI » URITHI WANGU SEHEMU 01

URITHI WANGU SEHEMU 01

2 Comments
SIMULIZI



                                                          
                                                               URITHI WANGU 


                                                       SEHEMU YA KWANZA


 Simulizi :       URITHI WANGU 
 Mtunzi :         RAJAB JK MWABUSEGA
Mawasiliano; +255 71653 8398

Siku zote katika maisha kuna kupanda na kushuka, pia viyu hivyo huo haupangi wewe mwenyewe pale unapopata shida au karaha ndani ya maisha yako ndipo vinatokea vitendo hivyo.
Binadamu tunayo sifa kubwa ambayo ni kurithi na sifa hiyo huwa inatokea ndani ya familia au katika ukoo, vitu huwa vinarithiwa, akili hurithiwa na kuna utata mkubwa katika kurithi mali na hakuna kipingamizi pale binadamu aporithishwa akili na mwenyezi mungu.Sio familia zote akili za wazazi hufanana na akili za watoto wao, nimeamini hilo kutoka kwa mama yangu mlezi aliye nilea tangu  nilipokuwa kichanga hadi kufika umri wa kujua baya na zuri.
Kuna mambo mengi aliyonitendea mama yangu mlezi, ila yalikuwa tofauti pale mnapokuwa nae yeye na ninapokuwa na watoto wake.Kulikuwa kuna siri kubwa kwa mama yangu mlezi ambayo sikuijua mimi na hata watoto wake hawakuijua, siku ilipojua siri hiyo niliona mwili wangu mzito.
Kwa kuwa tupo pamoja naomba twende sawasawia ili ujue mambo yaliyotokea na kisa nini hadi yanitokee mikasa ile, mkishajua itakuwa vizuri kuwafikishia ujumbe wale wenye tabia kama ya mama yangu mlezi wabadilike.
Japokuwa sikupata bahati ya kuonana na mama yangu mzazi nilipata habari kwamba nimefanana naye.Baada ya mama yangu kupata umauti, baba alichukua uamuzi wa kuoa mwanamke mwingine awe mrithi wa mama yangu mzazi ili nipate malezi yaliyo bora ya baba na mama.
Katika ndoa yao walibahatika kupata watoto wawili mapacha, mmoja wa kiume na mwingine wa kike.
Watoto hao maisha yao yalikuwa nje ya nchi ya Tanzania kimasomo.Ilikuwa kila baada ya likizo kubwa huwa wanarudi hapa nchini tanzani, wakiwa hapa huwa nakuwa na furaha pia upweke hunikimbia.
Mama yangu mlezi aliamua kuwaandikisha katika shule moja maarufu hapa nchini, ukaribu wetu ulikuwa umezidi kati yangu na wale wadogo zangu cha kushangaza mama yangu mlezi aliwakataza wasiwe karibu na mimi.Lakini kila atakachowaeleza nao lazima waje waniulize maswali kuhusu maisha ya pale nyumbani.
Nilipokuwepo chumbani kwangu nimelala, ghafla mlango nilisikia ukigongwa kwa hasira bila kusikia sauti ya mtu.Nilipofungua mlango nilivutwa kwa hasira huku nikipigwa makofi usoni mwangu.
“Aliyekutuma uende shule nani?” aliniuliza huku akinipiga makofi.
“Hajanituma mtu.”
“Nimesema sitaki nikuone umetoka humu ndani..”
“Ndiyo, nimekuelewa.”
“Nikisikia umeenda tena nitakachokufanya utajuta kuzaliwa..”
“Lakini mama….” alinikatisha kusema
“Lakini nini.? Na mimi si mama yako unasikia wewe paka..?”
“Mimi pia ni mtoto wako ujue hilo?”
“Sina mtoto kama wewe?”
“Nikufanyie kitu gani ili nipate upendo wako..?”
“Upendo wangu wanaostahili kupata ni watoto wangu tu.. na si
  wewe.?” mama yangu mlezi alinikata maini kwa maneno yake.
“Laiti kama watoto wako wangekuwa wanafanyiwa hivi,
  Kama wewe unavyonifanyia mimi ungejisikiaje..?”

2 Responses to "URITHI WANGU SEHEMU 01"

  1. Erick kabwe10 June 2019 at 20:16

    Nataka Nikusaidiye Mawazo Mawazo kidogo unahona kuhandika ukakiweka sokoni?

    ReplyDelete
    Replies
    1. abili8 September 2019 at 19:18

      Kimeshatimia na kipo tayari tatizo mtaji

      Delete
      Replies
        Reply
    2. Reply
Add comment
Load more...

← Newer Post Older Post → Home
Subscribe to: Post Comments (Atom)

FOLLOW US

POPULAR POSTS

  • KILA MWANDISHI WA MISWADA {SCRIPT}
    Kila mwandishi wa miswada {script} hutumia njia aipendayo kuitumia katika kuandika miswada {script}si kwa nchi yetu ya Tanzania pekee h...
  • IFAHAM HISTORIA YA KANUMBA YOTE KWA UJUMLA
    Hayati Steven Kanumba amezaliwa Januari 8 ,1984 Shinyanga,Tanzania Amefarki Aprili 7, 2012 (umri 28)Dar es Salaam,Tanzania Kaz...
  • SAMAKI MTU(MERMAID) 01
                                                                                                             SAMAKI MTU(MERMAID)   ...
  • MZEE MSISIRI ATUMBUA JIPU
    •••• ♦ •••• ♦ •••• ♦ •••• ♠ ••• ♦ 1. Jina langu kamili ni FADHILI RAJABU MSISILI 2. Kabira langu ni Chotara wa kizigua kwa baba na ...
  • SAMAKI MTU(MERMAID) 04
                                                                                                                          SAMAKI MTU(MERMAID...
  • ULINGO WA MOTO FILAM YA MAPIGANO YENYE UARISIA
    Daaah!!! Nikali tena ni noma sana,Usisa hau wala usikose kupata nakala yako.Tarehe 23/4/2018 filamu hii itakua tayari imo sokoni.....UL...
  • SAMAKI MTU(MERMAID) 02
                                                           SAMAKI MTU(MERMAID)                                                        ...
  • MFAHAM JUMA KILOWEKO SAJUKI
    Sajuki alizaliwa mwaka 1984, mkoani Songea na kupata elimu yake ya msing na sekondari hukohuko mkoani Songea.Ambapo mwaka 2005 aliweza ku...
  • JINSI YA KUTENGENEZA FILAM NA KUUZA
     KATIKA miongo kadhaa iliyopita filam nyingi zenye mafanikio zimetokezwa huko Hollywood. Hilo limekuwa na uvutano mkubwa ulimwenguni pote ...
  • SAMAKI MTU(MERMAID) 11
                                                                   SAMAKI MTU(MERMAID)                                                 ...
Back to top!
Copyright (c) 2014 FILM TANZANIA. All Rights Reserved Created by Flash TZ Blog. Designed by Flash TZ Blog. Powered by Blogger.