SAMAKI MTU(MERMAID)
SEHEMU YA NNE
Simulizi : SAMAKI MTU(MERMAID)
Mtunzi : Jackson James .
Mawasiliano; +255 762 892 472:, +255 652 064 958
Email: jamesjacson0@gmail.com
Mvua kubwa iliendelea kunyesha katika maeneo mengi ya marekani ikiwa ni pamoja na visiwa vya Mariana ,vilivyozungukwa na bahari ya pasifiki.chini ya bahari hiyo katika pango kubwa ,samaki mtu anaonekana akiwa amepumzika katika sehemu moja iliyoko pembeni ya pango hilo ,akiwa ameiweka mikono yake kifuani na kujikunyata katika maji ya chumvi na yenye baridi Kali siku hiyo kutokana na mvua kubwa iliyokuwa ikiendelea kunyesha katika visiwa hivyo. Mwishoni uvumilivu ulimshinda kutokana na kuhisi baridi kali kupindukia na haraka haraka aliamua kupiga mbizi ili kutoka nje maji hayo kwa muda,japo apunguze ukali wa baridi inayozidi mwilini mwake,alipiga mbizi mpaka akafika nje kabisa ya USO wa maji na kujivuta kuelekea ufukweni ,ingawa pia nchi kavu kulikuwa na baridi Kali iliyotokana na manyunyu yaliyokuwa yakiendelea kudondoka ,alifika nje kabisa ya maji akiwa ameishiwa nguvu kabisa na amezidiwa kutokana na baridi ile ,alijivuta na kusogea kabisa mchangani na kujilaza chini huku akitetemeka.
Baada ya kushindwa kurudi nyumbani asubuhi ile baada ya mvua kunyesha wakati akiwa katija safari yake aliyokuwa ameipanga kwenda sehemu alipomuona samaki mtu ,siku ya kwanza aliyoenda katika eneo la utafiti .James alikata shauri la kuondoka kurudi nyumbani baada ya kukaa ufukweni ,ndani ya gari kwa muda mrefu akisubiri mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha ikatike au kupungua ili aweze kuendelea na safari,ilipofika masaa ya SAA 11 jioni kwa saa za marekani,mvua ilipungua na kuisha kabisa,hii ilimpa kigugumizi James,cha kufanya maamzi hasa kuamua kwenda nyumbani ama kuendelea nasafari yake,aliwaza kwa muda ,kisha aka kata shauri la kuendelea na safari, hivyo alishuka na kuchukua vifaa vyake vichache alivyokuwa navyo kwaajili ya kuchukulia mambo muhimu,kisha akavaa koti kubwa la kumkinga na baridi kali ya siku hiyo,akaanza safari ya kuelekea katika eneo hilo maarafu ambalo linaogopwa na watu wengi,kwa kuhofia kuona maajabu ya kukutana na viumbe wa ajabu,baada ya dakika kadhaa alikuwa ameshakaribia katika eneo hilo hivyo akaanza kupiga hatua za polepole huku akijiimbia wa kupiga mluzi,kufurahia nyimbo nzuri aliyoipenda. Lakini ghafula wimbo wake ulikatizwa na taarifa ya macho iliyopelekwa ubongoni kwa haraka,baada ya kuona jambo la kushtukiza na kushangaza mbele yake,mwilini alitetemeka kwa hofu kwani hakutegemea kukutana na jambo hilo la 12
ajabu,alitamani aite watu lakini alipojaribu kuangaza hakukuwa na binadamu wa aina yoyote aliyeonekana japo kwa mbali katika muda huo.
************ ************
Mr David,alikuwa amepumzika ofsini kwake akiwa ameshikilia kipande cha karatasi mkononi mwake ,mawazo yake yalikuwa mbali kidogo bila kujua kwann amekuwa mwenye mawazo sana ,alichoka kukaa wima akaamua kunyosha miguu yake katika meza yake kubwa yenye vioo,na kichwa chake akakiegemeza kwenye kiti chake cha kifahari na taritibu alianza kupitiwa na usingizi, kabla ya simu yake ya mkononi haijaita, ngriiiiiiii,ngriiiii,ngriiiiii …….. Alipeleka mkono wake mahali ilipokuwa simu yake na kuishika kwaajilii ya kuipokea … “baba James ,tumepata mgeni nyumbani unaweza ukaja sasa hivi” ilikuwa ni sauti ya mke wake ., “aaah mke wangu mbona mapema sana kuna tatizo gani jamani,huyo mgeni ni nani” ,aliuliza mr David huku akijiweka sawa katika kiti chake, “ njoo basi utamuona ni MTU wa muhimu kweli” alijibu Mrs David ,huku akionekana kusisitiza hicho alichomwambia mmewe, “ sawa nakuja ndani ya muda mfupi “alimaliza mr David na kukata simu baada ya kuhakikisha mke wake ameridhika kwa majibu aliyompa.
******* *********
Anna ni msichana wa miaka 21,ni binti wa kitanzania ambaye yupo marekani kwa masomo ,ni mtoto wa tajiri mkubwa chini Tanzania ambaye pia anauhusiano wa kirafiki na familia ya mr David ambaye ndo baba mzazi wa kijana James,kwa muda mrefu tangu akiwa mdogo familia yake imekuwa ikimuandaa vizuri Ili aje aolewe na kijana wa familia ya mr David aitwaye James,ombi hill lilitolewa na wazazi wa james mwenyewe kutokana na wak kuhitaji mtoto wao kuoa msichana mtoto mwenye asili ya kiafrika ,japo hawakumshirikisha james isipokuwa Anna mwenyewe ndo alipewa taarifa hizi na kukubaliana Nazo kwa furaha kwani alikuwa na mapenzi ya dhati kwa kijana huyu tangu wakiwa watoto japo hakuweza kutambua kama James pia anampenda au laa.
“Aah karibu sana Anna” alisema mr David baada ya kufika nyumbani na kumuona mgeni aliyetarifiwa kwamba yupo. “asante baba shikamoo”alijibu anna na kusimama kisha kusalimia kwa heshima,”marhahaba ,habari za masomo?” aliiitikia mr David ,huku akimkabidhi mke wake begi lake ,alilokuwa ameshikilia mkononi, “masomo yanaenda vizuri ,pole na kazi baba”aliongeza anna huku akijiweka sawa pale alipokuwa amekaa. “nashukuru mungu kazi inaenda vizuri,rafiki yangu hajambo” aliongeza mr David huku akiagiza aletewe maji na mtumishi wake wa ndani, “ ni mzima anakusalimia sana”alijibu anna nakutabasamu, “sawa ni vizuri Anna , najua umemmsi sana James atakuja wiki ijayo “alisema mr James huku akitabasamu . “ kweli baba”?”aliuliza Anna kwa furaha, ” ndiyo ni kweli,aliongea nae kwenye simu wiki iliyopita” alidakia Mrs David huku akitabasamu, “Naamni akija pia atafurahi kukuona tena” aliongeza mr David .” asante baba nashukuru sana” alijibu Anna huku akishindwa kuzuia furaha aliyokuwa Nayo na kubaki 13
akitabasamu tu.Siku hiyo alishiriki chakula cha mchana na familia ya mr David’,na aliondoka jioni kurejea chuoni akiwa furaha baada ya kusikia taarifa za ujio wa James.
**************** **********
James alisogelea kitu kile kilichoonekana mbele yake kwa muda huo,ambacho kilionekana kumshangaza sana,baada ya kukosa cha kufanya na kubaki amesimama huku akiwa ametetemeka vya kutosha ,baada ya dakika kadhaa,akili yake iliwasaliana na ubongo na kuja na uamzi mzito uliopokelewa kwa mshangao na miguu yake ,ambayo kwa haraka iliamuliwa kutembea kuelekea katika eneo la tukio.alipiga hatua kadhaa na kukisogolea kwa ukaribu kitu hicho ,hakuamn macho yake alipoona kitu kile ni samaki MTU aliyekuwa na sura na nusu ya umbo binadamu wa kike,na alichoshangaa zaidi ni kuona sura ile ni ya msichana mrembo aliyemuona juu ya mwamba siku alipoenda kwa Mara ya kwanza kufanya utafiti lakini binti yule alipotea ghafla na yeye hakuwaza kwamba bintu yule ni samaki mtu, akili yake ilisimama kwa muda na asijue nini cha kufanya alibaki akimuangalia kwa mshangao ulio Changanyikana na huruma samaki yule,ambae kwa muda huo hali yake ilikuwa mbaya kutokana na baridi Kali aliyokuwa nayo kwa muda huo kiasi cha kushindwa kufumbua macho yake au kujisogeza kabisa pale alipokuwa alikuwa akichezesha mkia wake ambao ndo sawa na miguu yake,mikono yake ilikuwa imekunjamana kifuani kwake kama maiti iliyotayari kwa kuzikwa,sura yake nzuri na ya kuvutia iligeuka kuwa kama yenye majeraha ya siku nyingi kutokana na kuwa na michanga iliyokuwa imemganda katika kila sehemu ya uso wake.
Roho ya upole taratibu ilianza kumuingia james,macho yake yalionywa yasione kama kile kiumbe kilichopo mbele yake ni samaki mtu,Bali yaone ni binadamu wa kawaida,hivyo aliamua kumsaidia,.alishusha begi lake chini na kutoa nguo zake alizokuwa amekuja nazo kama za ziada aliamua kumvika shati lake samaki yule na kumfunga sehemu za kiunoni na suruali yake I’li kumsaida apate joto la haraka ,baada ya kuona hamna afadhali alimbeba na kumsogeza pembeni ya mwamba karibu na shimo lililopo chini ya mwamba huo, ambalo liko kama pango sehemu hiyo ilikuwa kavu kutokana na kuwa chini ya mwamba na maji ya mvua hayakuweza kupafikia ,alitoa tena jacketi lake zito na kumfunika nalo samaki yule jambo lile liliongeza afadhali na kumwezesha samaki yule kupata afadhali kidogo na kufumbua macho japo hakuwa na nguvu za kuamka,lakini alishangaa kujikuta hayupo majini,na yupo nchi kavu tena eneo ambalo hakujua amefikaje hapo,mbaya zaidi alipoangaza pembeni yake aliona kuna binadamu aliyekuwa akimuangalia kwa karibu,samaki mtu yule alijua yupo katika hali ya hatari hivyo aliamua kujinusuru , alirusha mikono yake pembeni na kufanya koti alilokuwa amefunikwa kuruka pembeni alizungusha mkia wake na kufanikiwa kutoa suruali,iliyokuwa imezungushwa kiunoni kwake,lakini kila alipojaribu kutoa shati alilokuwa amevikwa ilishindikana kwasababu hakujua namna ya kulito,alihangaika na kujilusha huku na huko lakini hakukuwa na mabadiliko,, . muda wote huo james,alikuwa akijiangalizia maajabu yaliyokuwa yakifanywa na samaki yule na alichukua pia kamera kwenye begi lake na kuchukua picha za kumsaidia katika utafiti wake, ila alipomuona kahangaika vya kutosha aliamua kusogea na kumsaidia japo ilikuwa ngumu kwa sababu samaki yule alikuwa akijurusha huku na kule ,akidhani anataka kudhuriwa na binadamu yule mwishowe akafanikiwa. 14
Baada ya kutolewa nguo hiyo,samaki MTU alijivuta kutoka mle pangoni huku akionekana mwenye hali mbaya sana lakini alijikaza na kuanza kufuata mchanga uliokuwa unaelekea baharini,alifanikiwa kutoka nje ya pango lakini nguvu zilimuishia baada ya kutumia nguvu nyingi kujivuta mchangani,alishindwa kuendelea japo akionekana kukaribia kuyagusa maji ,hivyo alijilaza akionekana kuchoka sana,alikaa kwa muda bila kusogea ,ndipo James alipomsogelea tena samaki yule na kumbeba kumpeleka majini muda huu samaki alitulia tuli huku akimuangalia james usoni, kuonyesha amekubali msaada wa rafiki yake huyo,alipofika karibu alimuweka majini na samaki yule alipata nguvu mpya ya kuanza safari yake ya kwenda makaoni kwake,James alifurahi baada ya kuona amefanikiwa kumuona kwa macho yake samaki MTU,na aliweza kupata picha ambazo zitamsaidia katika shughuli zake za masomo,alipohakikisha samaki MTU yule kapotelea baharini kabisa,alikusanya vifaa vyake akaondoka na kuelekea katika gari lake Ili aweze kurejea nyumbani kwani Giza lilianza kuingia katika maeneo yote ya kisiwa hicho na kufanya utulivu wa kutisha ufukweni pale.