SAMAKI MTU(MERMAID)
SEHEMU YA PILI
Simulizi : SAMAKI MTU(MERMAID)
Mtunzi : Jackson James .
Mawasiliano; +255 762 892 472:, +255 652 064 958
Email: jamesjacson0@gmail.com
Mwanga mdogo wa jua ulifanikiwa kupenya vioo,vilivyowekwa katika madirisha ya chumba cha James na kuongeza nuru katika chumba hicho kuashiria tayari ni asubuhi tulivu ya Siku nyingine ,katika siku hii James alilala kwa muda mrefu kutokana na kwamba hakuwa na ratiba ya 5
kwenda chuo kwa siku hiyo,kwani ilikuwa ni wikiendi,alijigeuza huku na huko huku akilaumu mwanga ulioonekana chumbani kwake kuashiria kum ekucha na inapaswa lakini bado alikuwa mbishi,alivuta blanketi lake zito na kuliweka vizuri katika mwilini mwake na kujigeuzia upande wa pili wa kitanda ili aendelee na usingizi lakini usingizi haukuja kama alivyopanga,kutokana na macho yake kuonekana makavu baada ya kukumbana na mwanga wa jua ambao kwa muda huo ulikuwa mkubwa zaidi chumbani kwake,alijigeuza tena upande wa kulia kisha kushoto halafu kulia tena ,kabla ya kutupa blanketi lake pembeni na kunyanyuka kwa uvivu kitandani,alijinyosha na kupiga miayo kadhaa,akatafuta viatu vya kukanyagia kwaajili ya kwenda bafuni kuoga na kufanya usafi alijivuta na kupiga hatua kadhaa kwenda kugusa kitasa cha mlango wa bafu uliopo chumbani kwake na kuingia bafuni kufanya usafi wake wa mwili.
Katika Siku hiyo James ,hakuwa na ratiba yoyote hivyo alipanga kwenda kutembelea maeneo mbalimbali ya ufuo wa bahari ya pasifiki hasa sehemu iliyosadikiwa ndo mahali ambapo viumbe vinavyosadikiwa kuwepo baharini japo havionekani kwa urahisi na kwa watu wengi,vilipokuwa vinapenda kukaa na kuota jua katika mida ya asubuhi au jioni,hivyo mbali ya James kutokuwa na uhakika wa kuviona au kukutana na viumbe hao,kutokana na kuaminika kupotea na kuangamizwa kabisa na sunami iliyoikumba bahari hiyo karibu wiki mbili zilizopita ,bado alihitaji japo kufanya uchunguzi katika eneo hilo ambao unaweza kumsaidia japo kuandaa taarifa fupi kuhusu ukweli wa kuwepo kwa viumbe hao hai ambao wanafanana na binadamu,kwani pia itamsaidia katika masomo yake yanayohusu elimu ya viumbe anayoyachukua sasa,”leo jioni nitaenda huko panaposemekana kulikuwa na viumbe hao wa ajabu’” alijisemea kimoyo kimoyo James,huku akiweka viungo vya chai katika maji yaliyokuwa yanachemka,kabla ya kushitushwa na mlio wa simu yake iliyokuwa mezani ngreee,….ngreee……ngreee…..ngreeee ….aliacha shughuli aliyokuwa anaifanya na kupiga hatua kuifuta simu yake na kuipokea..
“”hallow James hujambo mwanangu”ilikuwa ni sauti ya mama yake,.. “Ooh sijambo mama shikamoo” alijibu James akitabasamu ,kwani mbali ya kukulia marekani kwa miaka mingi lakini bado alimudu vyema lugha ya kiswahili ambayo Mara nyingi huitumia aongeapo na wazazi .. “vip hali ya masomo mwanangu “aliuliza Mrs David,.. ”naendelea vizuri mama nitafaulu India shaka”alisema James kwa kujiamini huku akipunguza kasi ya moto katika jiko kubwa analolitumia.. “sawa Fanya haraka uje huku utuone na sisi tumekumiss”alisema kwa furaha Mrs David,…. “sawa mama baada ya mwezi huu nitakuja kuwasalimia huko newyork” alijibu James kwa mkazo kuonyesha atatimiza hicho alichomuhaidi mama yake, “sawa masomo mema mwanangu kwaheri” alimaliza Mrs David na kusubiri jibu la mwanae kabla ya kukata simu. . “sawa mama kazi njema pia,msalimie baba ,”alimaliza pia James ,”sawa nitamkumbusha akupigie pindi akitoka kazini” alijibu mama kwa mkazo kusisitiza alichokiongea . “sawa mama”alijibu James na simu ikakatwa.
Katika kipindi chote tangu azaliwe James amekuwa akipendwa zaidi na wazazi wake kuliko watu wengine ambao walikuwa wanamzunguka,hii ni kwa sababu huko marekani hakuwa na ndugu wa aina yoyote zaidi ya marafiki na majirani ,ndugu zake wa upande wa baba na mama walikuwa nchini Tanzania,japo James awafahamu na wao awamfahami James kwani wazazi wa James 6
waliondoka Tanzania kuja marekani ,James akiwa na umri wa miezi 7 pekee ,hivyo ni vigumu kumkumbuka alivyo mpaka sasa akiwa ni kijana .
Baada ya chakula cha mchana James,aliandaa vizuri begi lake lenye vifaa mbalimbali vitakavyomsaidia katika uchunguzi na utafiti wake,pia aliweka nguo za ziada endapo kama itatokea dharura itakayomlazimu kubadili mavazi aliyoenda nayo,mwisho alichukua maji na vinywaji vingine vya kupooza koo awapo katika shughuli hiyo nzito.alijiweka sawa na taritibu akaliinua begi lake ambalo lilionekana zito kiasi kabla ya kuliweka mgongoni kwake ,kisha akapiga hatua taratibu kuelekea mlangoni na kufungua kitasa cha mlango na kuurudishia kwa nguvu kisha kuufunga kwa funguo maalumu ,haraka haraka akapiga hatua kuelekea lilipopakiwa gari lake akaweka begi alilonalo mgongoni katika siti ya nyuma na kuwasha gari kuelekea ufukweni..
Baada ya kukaa majini kwa muda mrefu ,samaki maarufu kama samaki MTU aliamua kutoka nje ya maji kwenda katika mwamba mkubwa kwenye ufuo wa bahari ,ambapo ndipo mahali anapopenda kukaa na kupumzika Mara kwa Mara,alipiga mbizi taratibu kuelekea juu ndani ya dakika chache tu alikuwa amefika nje kabisa ya maji na alijivuta taratibu kuelekea kwenye mwamba uliokuwa pembeni mwa ufuo wa bahari na kupanda kiasi mahali alipoona anaweza kuwaona maadui wake wote wanaoweza kumsogelea,alipojiridhisha na usalama wa mazingira aliyokuwemo akajilaza huku mkia wake ambao ndo sawa ni miguu yake ukiyachezea mawimbi madogo ya maji yaliyokuwa yakijaribu kupanda katika mwamba.
Kutokana na mizunguko ya siku nzima na kazi nzito zilizomuandama siku ya wikiendi ,millian alijikuta akilala kwa muda mrefu japo ilikuwa ni muda wa alasiri ,alikuja kushitushwa na mwanga wa jua ambao ulifanikiwa kupenya katika dirisha na pazia lililowekwa kuzuia mwanga ,na kuja kumchoma katika paji lake la uso kwa Mara ya kwanza alijitahidi kuvumilia hali ile lakini ilimzidi nguvu hasa mwanga ule ulipozidi kuongezeka na kuwa mkubwa kila jua lilipo sogea,alijivuta taratibu na kusogea pembeni kabisa mwa kitanda Ili kuukwepa mwanga ule lakini ni kama alifukuza kabisa usingizi aliokuwa nao hivyo aliamua kuamka na kuendelea na kazi nyingine za nyumbani,wakati akijiandaa kuamka Mara alikumbuka kwamba katika siku hiyo nzima hajakutana wala kuongea na kijana aliyempenda sana aitwaye James,huyu ndo MTU pekee ambaye anampenda kwa dhati japo hakupata nafasi ya kuziwasilisha hisia zake kwake.baada ya kuwaza kwa muda alifikia uamzi wa kumpigia simu ,lakini simu yake iliita bila kupokelewa ,alirudia Mara kwa Mara lakini majibu yalikuwa ni Yale yale.,hali hii ilimtia wasiwasi ,,” what wrong with him today”(nini tatizo alilonalo Leo) aliwaza millian,aliamua kutulia kwa muda kisha akaamua kujaribu kupiga tena na tena lakini hakukuwa na jipya katika hilo,hali ilimfanya ajihisi vibaya na kukosa hata nguvu ya kunyanyuka kama awali alivyopanga,mwanga wa jua uliopenya na kumuumiza aliona ni kama kiyoyozi kizuri kilichomburudisha hivyo hakuona hata sababu ya kuendelea kuukwepa tena,aliamua kusogeza mto wake mkubwa uliokuwa kitandani kwake na kuegemeza kichwa chake chenye nywele laini juu yake,huku akiangalia juu kama MTU anayehesabu idadi ya vitu anavyoviona katika Dari ya chumba,lakini mawazo yake yalikuwa mbali sana kiasi kwamba hakuweza kuona hata kitu chochote kilichokuwa katika Dari ya chumba kile licha ya Dari hiyo kujazana na vitu vya thamani na vinavyovutia kutazama ,wishowe alipitiwa tena na usingizi ambao 7
hakuutegemea katika kipindi hicho,akalala mpaka pale aliposhituliwa na sauti ya mdogo wake wa kiume.”sister wake up please, am tired to be alone” (dada amka Tafadhali nimechoka kuwa pekee yangu) ilikuwa ni sauti johonson akiomba dada yake aamke.”ok am coming my young” (sawa nakuja mdogo wangu) alijibu milliani kwa sauti ya uchovu nakujitahidi kunyanyuka huku akijinyosha na kupiga miayo mikali iliyoashiria uchovu mzito alionao.
************* ***********
Gari ndogo ya kifahari iliapaki katika eneo la pembeni kidogo mwa ufukweni mwa bahari mahali palipokuwa pametulia kabisa kutokana na kuwa na idadi ya watu wachache waliokuwa wamepumzika na wengine wakichezea maji ,James alishuka katika gari na kuanza kuangaza huku na huko kabla ya kutafuta mahali pa kuanza kufanyia kazi ,japo eneo kuu lililokuwa akilini mwake ilikuwa ni sehemu ambayo husadikiwa kuwa na viumbe wa ajabu ambo ni samaki watu.alipiga hatua kadhaa na kuangalia mawimbi ya maji yaliyokuwa yakienda na kurudi ,baada ya dakika kadhaa alirudi katika gari yake na kuchukua vifaa alivyoviandaa katika begi na kisha aliliweka mgongoni na kurudishia mlango wa gari na kuhakikisha kama umefungwa vizuri ,akaanza kupiga hatua za haraka kuelekea katika sehemu inayohisiwa kuonekana kwa samaki watu katika siku za nyuma,ambayo ilikuwa iko umbali wa nusu saa kwa kutembea kwa kasi stahiki .alitembea akifuatisha ufuo wa bahari na kwa muda mfupi tu akaanza kuchoka na kuhisi kiu,aliamua kushusha begi lake chini na kuchukua maji ya kunywa aliyokuwa ameyaandaa na kunywa harakaharaka,kisha alirudisha yaliyobaki na kuyahifadhi katika begi na kulifunga vizuri tayari kuendelea na safari ambayo ilionekana ndefu kinyume na matarajio yake na namna alivyoelekezwa lakini alikuwa amebakiza dakika chache tu kufika hapo.
Baada ya kukaa kwa muda katika mwamba huo anaoupenda tangu akiwa mdogo ,ambapo alikuwa akikaa kwenye mwamba huo akiwa pamoja na ndugu zake ambo waliangamizwa na sunami katika kipindi cha nyuma,samaki mtu aliamua kurudi katika maji lakini wakati akijiandaa kushuka katika mwamba huo aliokuwa amejilaza alisikia sauti ya mtu ,ambayo ilionekana ipo karibu zaidi na nijambo ambalo hata yeye hakulitarajia,”hey miss what are you doing there?”(habari mrembo unafanya nini hapo?) Ilikuwa ni sauti ya kiume ambayo iliongea kwa uchovu,hii ilikuwa ni sauti ya James ambaye kwa muda huo aliamua kutua begi lake chini ili asogee juu ya mwamba akutane huyo mrembo ambaye angeweza hata kumsaidia hata katika kufanya utafiti wake.samaki MTU baada ya kusikia sauti ya binadamu tena wa kiume ikiongea karibu yake aligeuka na kuangalia Mtu huyo anayemuongelesha yupo upande gani,lakini aligundua kwamba MTU Huyo ameinama na anatoa begi lilipo mgongoni,aliona hatari kubwa itakayomkabili kama mtu huyo akimaliza kuweka begi lake chini na kupanda juu yamwamba ,hivy aliamua kutumia nafasi ya MTU Huyo kuinama yeye alijivuta kwa haraka haraka na kujitupa baharini……. pwaaaaa(mlio wa sauti ya maji) ,,.
James alikuwa amemaliza kuweka sawa vifaa vyake kabla ya kuona kitu kama mkia wa samaki mkubwa ukipotelea katika bahari ,alishituka sana lakini kilichomshangaza zaidi ni kuona kama sehemu ya mbele ya kiumbe hicho ni umbile la binadamu,alibaki akiangalia mawimbi madogo ya 8
bahari,yaliyosindikiza maajabu yaliyoonekana katika muda huo ,kiukweli hakuamini kabisa kukutana na kiumbe cha ajabu ambacho ndicho hasa kilichomfanya kufunga safari kuja katika mazingira hayo ,alipigwa na butwaa kwa muda kisha akatabasamu na kuona kwamba sasa atafanikiwa katika malengo yake ya Mara akakumbuka kuna msichana mrembo aliyekuwa juu ya mwamba ,akaamini Huyo ndo atamsaidia katika kumpa maelezo juu ya viumbe hawa kwani isitoshe na yule msichana atakuwa ameona tukio la kuonekana ten kwa kiumbe wa ajabu aina ya samaki mtu ,alitabasamu tena na kusema kwa nguvu”hey miss did you also see that mermaid?”(mrembo je na wewe umemuona samaki MTU?)aliuliza James huku akitegemea kupata majibu stahiki kutoka kwa MTU aliyemuuliza lakini haikuwa hivyo zilipita sekunde kadhaa zilizokaribia kuunda dakika nzima bila majibu yoyote,alipogeuka na kuangalia katika mwamba huo hakuona MTU wala kitu chochote kilichokuwa mahali hapo ,aliangaza huku na huko lakini pia hakufanikiwa kuona kitu.” Atakuwa amekwenda wapi tena?”alijiuliza kichwani bila majibu yoyote .mwisho akaamua kuita “hey miss”(wewe mrembo) alirudia na kurudia lakini hakukuwa na MTU wa kujibu au kusikia sauti yake kutokana na eneo hilo kuwa mbali kidogo na mazingira ambayo hufikiwa na watu wengi.”lakini kama angeondoka si ningemuona japo kwa mbali “alijisemea james huku akijaribu kutafakari lakini bila majibu,kwa akili yake changa ilikuwa ni vigumu kuamni kama mrembo yule aliyekuwa juu ya mwamba ni samaki mtu ,hivyo alitoa uamzi usiokuwa na busara ya kutosha na kujisemea”labda kaogopa alipoona samaki MTU na kuamua kukimbia” ,,,baada ya kutoa uamzi huo aliona ni vyema kumilisha shughuli yake iliyompeleka hapo ikiwa ni pamoja na kupiga picha na kuandaa taarifa yake ,juu ya uwepo wa samaki wa ajabu aina ya samaki watu.alipokamilisha kufanya vitu vya msingi alivyovihitaji alikusanya vifaa vyake na kuvirudisha katika begi kisha alilibeba mgongon mwake na kuanza safari taratibu,huku akionekana mchovu na kurudi mahali ilipo gari yake ,njia nzima aliwaza namna alivyokiona kiumbe cha ajabu kikipotela majini lakini pia akusahau picha ya mrembo aliyekuwa katika mwamba kabla ya kupotea ghafla.” Alikuwa mrembo kweli” alijisemea James huku akitabasamu na kuongeza kasi ya gari lake…