SAMAKI MTU(MERMAID)
SEHEMU YA TATU
Simulizi : SAMAKI MTU(MERMAID)
Mtunzi : Jackson James .
Mawasiliano; +255 762 892 472:, +255 652 064 958
Email: jamesjacson0@gmail.com
Mbali na kuwa mfanyabiashara maarufu na MTU tajiri katika kisiwa cha Mariana, lakini pia Mr Richard alikuwa ni MTU asiyependa mchezo na katili na aliogopeka sana katika kisiwa hicho ,kutokana na kutoa adhabu Kali kwa watu waliokuwa wanacheza na Mali zake au familia yake,yote haya aliyafanya akiwa na vijana wake wa kazi ambao walitekeleza kazi yoyote ambayo waliagizwa na Mkuu wao.japo alikuwa ni MTU wa aina hiyo lakini bado aliipenda na kuithamini familia Yake ,yeye kama baba wa familia hiyo pekee.
Ngriii …ngriii …ngriiii… mlio wa simu iliyokuwa mezani kwake ilimfanya Mr Richard ,aache shughuli aliyokuwa akiifanya na kusogeza mkono wake mahali ilipo simu yake ya mkononi na kupokea “hellow dad its time for lunch now ,can you came home as soon as possible (halo baba ni muda wa chakula cha mchana sasa ,unaweza ukaja nyumbani haraka kama iwezekanavyo)" ilikuwa ni sauti ya millian,ikimsihi baba yake.”oooh my daughter am bucy now, I 9
have some jobs to finish off but one hour to come ,I will be there”( oooh mtoto wangu nipo bize kwa sasa ,ninakazi kidogo ya kumalizia lakini nitakuwa nyumbani ndani ya SAA moja lijalo” )alijibu Mr Richard huku akitabasamu. “ok my dad I will exactly stay waiting for you” (sawa baba yangu ,nitakaa nikisubiri ujio wako) alijibu millian ,kwa matumaini makubwa ya kile alichohakikishiwa na baba yake.”ok see you there my daughter byee”(sawa mtoto wangu nitakuona hapo kwaheri )alimaliza Mr Richard na kukata simu. “ok bye dad” (sawa kwaheri baba) alimaliza pia millian.
Mr Richard baada ya muda mfupi alimaliza kazi zake hivyo alipanga vitu vyake vizuri ili akamuone mtoto wake na familia yake kwaajili ya kushiriki chakula cha mchana, alinyanyua simu yake ya mezani nakumpigia msaidizi wake. . “ am on my way to home ,please finish the rest of work here”(naelekea nyumbani sasa Tafadhali maliza kazi zilizobakia hapa) alisema mr Richard na kusibiri jibu upande wa pili . “ok boss” (sawa bosi) ilijibu sauti ya upande wa pili na simu ikakatwa.alichukua begi lake Dogo na kuanza kupiga hatua kuelekea nje ya jengo kubwa la ofsi yake na kuelekea mahali gari yake ilipo ,akaliwasha na kuondoa kwa kasi.
********* ***********
Kutokana na uchovu aliokuwa nao kutokana na safari ya Jana,James alijikuta akilala mpka alipokuja kushtuliwa na mlio wa simu yake iliyokuwa ikimkumbusha kwamba ni muda wa kufanya mazoezi ya mwili,ilibidi atii mlio huo aliouweka mwenyewe katika hiyo simu yake ili imuwezeshe kukumbuka kufanya mazoezi ya viungo kila siku kwaajili ya afya yake,alijivuta na kuliweka shuka lake pembeni Kisha akapiga miayo kadhaa ,akashusha miguu yake chini ya kitanda chake kikubwa ,hakuweza kupata usingizi mzuri kutokana na uchovu na mawazo mazito juu ya kile alichokiona Jana, lakini pia mawazo yake hayakuisha kumkumbuka mrembo ambaye alimuona ,alipokuwa ameenda kufanya utafiti juu ya viumbe wanaosadikiwa kuwepo na kuishi baharini , lakini pia alifanikiwa kumuona mmoja wa samaki hao. Sura ya mrembo huyo ilikuwa ikizidi kumjia akilini kila alipofikiria safari yake hiyo ya Jana,lakini kinachomshangaza zaidi ni hatumbui ni wapi yule mrembo alipoenda kwani ilikuwa ni ghafla sana ,kwani hata angeondoka ni lazima angemuona akitoka ,bado hakutaka kuwaza kwamba yule mrembo aliyemuona ndo samaki mtu ambaye alifanikiwa kuuona mkia wake ukipotelea baharini,”atakuwa alipita wapi ?” aliwaza James bila majibu yoyote,mwishowe alijivuta kwa nguvu kitandani na kukanyaga chini akaweka miguu katika viatu vya kukanyagia na kuelekea bafuni kufanya usafi kabla ya kwenda kufanya mazoezi ya viungo .kwa kuwa siku hiyo hakuwa na ratiba maalumu aliamua kupmzika nyumbani na kufanya kazi za pale,hii ni kwa sababu alikuwa anaishi peke yake na hakukuwa na mfanyakazi wala MTU yoyote wa kumsaidia kazi hizo,alianza kwa kusafisha nyumba nzima na kufuta vumbi kwenye vyombo na maeneo mengine ya nyumba kisha akamiliza kwa kufanya usafi katika maeneo ya nje,na alipojiridhisha kwamba ametimiza kile alichokihitaji ,akaingia chumbani na kwenda kubadili mavazi tayari kwenda kuoga,ili kuondoa uchovu alionao kutokana na kazi ngumu alizozifanya kwa siku hiyo,alipiga hatua kuelekea mahali bafu lilipo,alipokuwa amegusa kitasa tayari kwa kufungua mlango wa bafu,alisikia alamu ya mlango ikilia kuashiria kuna MTU mlangoni anahitaji kuingia ndani,”mmmh huyu nani tena” alijiuliza James,kwa sababu hakumualika MTU 10
yoyote kuja kumtembelea kwa siku hiyo na wala hakupokea ombi la mtu kuja kumtembelea ,aliondoka kwa kasi kutoka chumbani na kushuka ngazi kwa haraka na kupiga hatua kuufata mlango ulipo alipoangalia kwenye kamera ya mlangoni aligundua aliopo mlangoni si mwingine ila ni binti wa kizungu ambaye ni rafiki yake wa karibu aitwaye millian, “”oooh millian welcome” (aahhh millian karibu)alisema James ,huku akitabasamu na kuonyesha mshangao kutokana na ujio wa ghafla wa mgeni yule, “thank you much ,are you fine James”(asante sana,haujambo James ) alisema millian,huku akijiandaa kuingia ndani kama akivyotakiwa na mwenyeji wake, “yeah am fine,how a bout you”(ndio Mimi sijambo VIP kuhusu were?)Aliuliza James huku akiweka vizuri taulo yake kiunoni kwani alikuwa amekwisha jiandaa kuelekea bafuni, “aaahh well am fine too but not that much” (aah ndiyo Mimi sijambo pia ingawa sio sana ) aliongea millian kwa aibu ,hasa alipo angalia kifua cha James ,kilichokuwa kimejazana na kutengeneza umbo kamili la mwanamume mwenye nguvu,James aligundua aibu iliyomkumba millian hivyo akaamua kumuomba amsubiri ili akaoge mara moja,ombi ambalo millian alilipokea kwa furaha japo hakutaka kuionesha wazi kwa James,…japo si Mara ya kwanza kwake kuja nyumbani kwa James,lakini ilikuwa ni Mara ya kwanza kumuona James katika mazingira kama hayo yaliyofanya mwendo wa moyo wake kubadilika ghafla kutokana na kumpenda kwa dhati kijana Huyo ambae hapendi sana kuwa mahusiano ya kimapenzi ,hii ni kwa sababu hakuhitaji usumbufu hasa katika kipindi hiki alicho masomoni. Alimuacha millian sebuleni baada ya kumpa kinywaji alichohitaji na kisha akapenda ngazi haraka haraka kuelekea chumbani ili aweze kwenda kuoga,alitumia dakika chache tu kuoga akatoka bafuni na kuingia chumbani kujiandaa na kubadili mavazi haraka haraka ili aepushe kumkera mgeni wake anayemsubiri sebuleni,alivaa shati ya mikono mirefu iliyomkaa vyema,na akavaa suruali aina ya jinsi aliyoipenda,na haraka haraka akashuka ngazi kwenda sebuleni ambako alimkuta mgeni wake akiwa amejilaza kwenye sofa akionekana mwenye mawazo mengi, “oooh did you wait that much”(utakuwa umesubiri sana ?)aliuliza James,huku mguu wake wa kulia ukimaliza ngazi ya mwisho na kukanyaga kapeti la ssebuleni. ”aahh not that much”(hapana sio sana)alijibu millian akinyanyuka mahali alipojilaza na kuelekeza USO wake kwa James.
“whats wrong with you,now days James”(nini tatizo lako katika siku hizi )aliuliza millian ,baada ya kuona ukimya wa muda mrefu kutoka kwa mwenyeji wake ambaye muda huo alikuwa akifurahia kipindi cha televisheni ,kilichokuwa kikionyesha katuni. “”oooh nothing special,what’s up” (aaha Hamna jipya ,kwanini kuna tatizo?)aliuliza James,nakuacha kuelekeza macho kwenye kile akichokuwa akikiangalia na kumuangalia milliani usoni, “you didn’t pick my phone,several times from yestarday” (hukupokea simu yangu kuanzia Jana)alisema millian huku akionekana kuyakwepa macho ya James,yaliyokuwa yameelekezwa kwake kwa dakika kadhaa. “aah sorry millian,I don’t have special reasons for me to do so ,but I was very bucy from yestarday” (samahani milliani ,sikuwa na sababu ya muhimu ya Mimi kushindwa kufanya hivyo ,lakini nilikuwa bize sana toka Jana) alijibu James kwa upole huku akigeuza macho yake kuelekea pembeni. “ok I was just afraid ,that you may have something bad with you” (sawa nilikuwa naogopa tu kwamba unaweza kuwa kuna kitu kibaya kimekupata) aliongea millian kwa unyonge akionyesha wazi kutofurahia kitendo cha James,kutopokea simu yake bila sababu,kwa kuligundua hilo james,alimshika mkono milliani na kumnyanyua kwa nguvu pale alipokuwa amekaa kisha kumvuti 11
kifuani kwake na kumkumbati msichana yule wa kizungu ambaye moyo wake ulienda mbio kupita maelezo baada ya kuhisi joto la mwanamme ampendaye kwa Mara ya kwanza mwilini mwake.
Siku hiyo millian alipata nafasi ya kushinda na James,nyumbani kwake kwa muda mrefu wakipata nafasi ya kucheza ,kula pamoja na kufanya shughuli nyingine za chuoni kwa pamoja,ilipofika majira ya jioni millian aliamua kurudi nyumbani huku akionekana mwenye furaha kwa kufurahia mambo yote aliyofanya na James wakiwa pamoja lakini hasa alitabasamu akikumbuka namna James alivyomkumbatia kwa nguvu, “finally you have understand my feelings James”(hatimaye umeelewa hisia zangu James) alijisemea huku akitabasamu millian wakati akiwa anaendesha gari yake kueleke kwao.
• SAMAKI MTU