Script ni nini?
Mwandishi mzoefu lazima ajue maana ya script kwa lugha yetu inaitwa mswada,wengine hupenda kuita muongozo wa filam.Script ni maandiko yenye uchambuzi kila tendo au tukio la kisauti au kitabia yenye kuonekana katika kueleza hadithi(story).
Filam inategemea utendaji wa watu zaidi ya mmoja ili kukamilika nao ni mtunzi wa story,mwandishi wa story,mtayarishaji wa story,muongozaji wa story, wapigaji picha wahusika na wengine wengi kutokana na bajet(budget) ya filam hivyo bila karatasi au document yenye maandiko yaliyo chambuliwa na muongozo wa story inakuwa ngumu kumuelewesha muhusika kuhusu story inayotakiwa kuitendea vitendo,nchi zilizo endelea au watendaji walio makini wanaipitia script ili kufaham story nzima inavyokwenda na inahusu nini?.
Kwa njia hii ni rahisi kwa wahusika kuuvaa uhusika unaotakiwa atakuwa ameilewa nafasi yake kwa marefu na mapana.Muhimu kufahamu filam yako ni maalum kwa walengwa wapi usisahau hao walengwa lazima uoneshe story yako wakae kwa muda kuipitia kama itakuwa kuna sehemu hajaielewa akuulize sio awahadithie alafu siku ya kuanza kazi ndio awapatie script, Pia script yako unatakiwa uichambue vitu ambavyo vinaweza kuonekana na walengwa au watazamaji [audience] sio wasikie vikihadithiwa.
Uandisshi wa muongozo wa filamu muswada [script] unatakiwa unao vitu vya kuonekana au kuoneshwa kuliko kuhadithiwa au kusikika [mfano] Muhusika anamuhadithia tukio alilolipata au aliloliona likiwa katika hiyo filamu hilo tukio halijaoneshwa,kinyume chake itapelekea story yako kutokuwa na mvuto kutokana na simulizi nyingi kuliko vitendo vyenyewe vinavyosimuliwa ndani ya hiyo filamu. Siku zote filamu ni sanaa inayoonyesha story ya mtu au kitu ili filamu ipendwe lazima iwe na story nzuri wahusika waitendee haki kama tukio linalofanyika kweli hata mtazamaji akimaliza kuiangalia awe amehusika kwa kuifikiria na ajiulize kama angekuwa yeye pia asijilaumu amepoteza pesa kuinunua filamu yako. Story nyingi zipo ndani ya kanuni na kanuni yake ndani ya story lazima awe muhusika na hitaji.Muhimu kuweka kisa kizuri kionekane kina uhalisia zaidi ili iwe rahisi kueleweka kwa walengwa wako,kisa chako kimpelekee mhusika mkuu kukaa katika nafasi yake na kuwashawishi watazamaji kumpenda na kumwonea huruma au kumpongeza kwa utendaji wake mzuri katika hiyo filamu hapo ndipo kwenye moyo wa filamu.
Kisa ni kitu kinampelekea muhusika wako mkuu asifikie lengo lake kwa mikiasa na misukosuko anayoyapata muhusika wako mkuu usimpeleke haraka katika lengo lake lazima upitie majaribuni nao watazamaji wa filamu wanyanyuke kwa hisia hapo ndipo mtazamaji ataacha shughuli zake na kuwa mkini katika hiyo filamu baadhi watazamaji wanaokuwa wapole hata kuongeleshwa hataki, hakikisha unakuwa na visa vidogo vidogo ambavyo vinazaa matukio yatakayomfanya muhusika wako mkuu anazidi kudidimia, kila atakaposhika kwa moto huruma na upendo kwa muhusika mkuu utatoka kwa watazamaji.
Filamu itakuwa na mvuto zaidi kama utapangilia vizuri visa na mtiririko mzuri wa mtukio halisi yenye kuvutia na kutomtoa muhusika mkuu katika lengo lake kuu na sio mbaya ukawaweka watu watakao msaidia muhusika mkuu katika lengo lake hao wasaidizi wake watamwongezea nguvu katika hitaji lake ila usimkimbizishe au kumtoa kwenye tatizo ulilomwekea.Kisa hiki ni kitendo au tukio lolote ambalo linaloongezeka na kuleta vizuizi upingamizi na ugumu katika safari ya kufika katika lengo ambalo ndilo hitaji la muhusika kwa kuzingatia vitu hivyo tutazame muundo maarufu sana katika uandisi wa miongozo ya filamu, muundo huu pia hutumika katika uandisi wa vitabu vya tamthilia riwaya na michezo au maijizo ya luninga kufahamika three act structure [vitendo vitabu vya muundo]. Mfano