Vitu
vya kuzingatia unapohitaji kuandika story ya filamu kabla ya kuandika
kuna vipengele lazima upitie uweze kukamirisha story. 1. Wazo yaani aina
ya story namaanisha story ya aina gani uandike.
2. Muhusuka wako jinsia
gani, umri gani, tabia yake, kazi yake anayoifanya, anayo familia au
ana familia nk. 3. Muhusika wako analo lengo gani katika hiyo story nini
azma yake Mfano:- kufuatilia mauaji, anatafuta kazi ili aweze
kujikwamua kimaisha.
4. Lazima tuone vikwazo anapokaribi
a
kufanikiwa au kufanikisha lengo lake kitatokea kikwazo hapo ndipo
unapata msisimko wa filamu hapo katika kikwazo ndipo tunapata adui au
maadui wake na huyo hadui anaweza kuwa mtu, jini au hata mazingira na
hata njaa pia ni adui.
5. Lazima atatue kikwazo atakabiliana vipi na
adui.
6. Majibu yote yapatikane katika story yako muhusika wako
atafanikiwa au hatofanikiwa, tujifunze katika filamu za wenzetu zipo
steering anakufa adui anabakia ina maana steering ameshindwa kukwamua
tatizo na Mara nyingi vikwazo kama hivi adui anayo nguvu nyingi au akili
nyingi za kupambana na steering, hizi ni hatua za mpanfilio wa story.