MUIGIZAJI MZURI KUPATIKANA KWAKE
Kuna vitu vya kuvizingatia ili kumjpata msanii mzuri bila sekata tano kushirikiana haiwezekana kupatikana msanii mzuri.
Story na script zipangiliwe vizuri na zisisimue (Uandishi.)
Mkurugenzi, uongozi (director) mzuri.
Upigaji picha (camera) uliotulivu.
Uzalishaji, utayarishaji (production).
Mwigizaji mwenyewe/
Msanii kuigiza vizuri na kuwavutia watu wanaotizama sio kazi yake mwenyewe mwigizaji bali ni kazi ambayo inahitaji msaada kutika kwa zilizotajwa hapo juu.
UANDISHI (STORY NA SCRIPT ZIPANGILIWE VIZURI)
Ili story na script zipangiliwe vizuri nazisisimue ni lazima mtunzi wa story na mwandishi wa script wawe wabunifu na hiyo kazi iandikwe kwa ufasaha ikiwezekana itafsilike vizuri katika lugha ya sauti na picha ni vizuri mwandishi wa script atoe nafasi ya waigizaji kuonesha uwezo wao halisi nao wahusika.
MKURUGENZI, UONGOZAJI (DIRECTOR) MZURI
Director anayo kazi kubwa ya kuwaongezea wasanii na mpiga picha haswa tuzungumzie kwa wasanii,director lazima ashilikiane na casting ili iwasaidie kuwaweka vizuri wasanii kwa lugha zitakazo tumika katika script.Timu ya uchaguzi kwa wasanii inatakiwa ichague wasanii watakaofaa kujijaza nafasi zilizoumbwa na mwandishi wa mswada(script) na hadithi(story) ni vema msanii anayechaguliwa katika uhusika Fulani awe kweli mwenye uwezo wa kuicheza nafasi hiyo na sio uchaguzi ufanyike kutegemea sababu dhoofu, kazi ya kuuvaa uhusika ni rahisi ambapo muigizaji na ule uhusika unashabihiana.Muongozaji(Director) ni lazima aisome story na script mapema na kuielewa endapo ajaielewa lazima akae pamoja na mwandishi ndipo achukue jukumu kuiruhusu kazi ifanyike na kuisimamia.
UPIGAJI PICHA (CAMERA)
Wanaohusika na upigaji picha wanao umuhimu mkubwa msanii anamtegemea mpiga picha kuna sehem nyingine mtu wa kamera hupata kazi sehemu ya shoti na sehem nyingine.Mpiga picha akiwa sio mtulivu hatoweza kutoa video nzuri nailio tulia,utulivu ni swala kubwa analotakiwa kuwa nalo mpiga picha.
UZALISHAJI, UTAYARISHAJI (PRODUCTION)
Nitoleo muhimu la script lililotayari kwa utayarishaji wa filam ikijumuisha pamoja maelezo ya kiufundi(techinical instruction) kama vile maelezo ya uhariri wa filam upigaji picha na mambo kama hayo kosa kubwa la mwandishi mchanga(spec script writer) wa filam.Production inayomajukum yake kama mpiga picha alivyokuwa anayomajukum yake.
MUIGIZAJI MWENYEWE
Muigizaji amezungumziwa sana lakini tukumbushie kidogo,muigizaji anatakiwa aitendee haki nafasi aliyopatiwa awe ameuvaa uhusika uliousoma katika script aliyopatiwa.