Kama kawaida najisikia kuandika kuhusu Tansinia ya filamu
Tanzania....unamkumbuka Mc Napo ....!? jamaa anajulikana kwa jina
la Ernest Napolione pichani sidhani kama jamaa kuna kitu aliacha
kutoka kuwa Dj mpaka mtangazaji na rapper wa bongofleva na miaka ya
karibuni filamu huyu jamaa muigizaji aliyezaliwa nchini Urusi na
kuingia Tanzania akiwa na miaka 5 baba yake ni Mtanzania mama yake
ni Mrusi filamu yake ya kwanza kuigiza akiwa na miak
a
3 na jina la filamu hiyo iliyotengenezwa nchini Urusi iliitwa New
year in the Old soviet union baadaye Going Bongo
iliyomtambulisha
na Kiumeni (pichani baadhi ya matukio katika filamu hiyo)
huyu
jamaa amesomea masomo ya sayansi ya computer na baadaye uandishi
na utaarishaji filamu nchini Marekani katika jiji la Los Angeles
kwasasa kikubwa jamaa ni Rais wa kampuni kubwa ya filamu D street
kazi yake kubwa ni kusimamia filamu katika bara la Afrika na
Afrika mashariki hapa ndiyo lengo la makala hii ilipo mpaka
sasa nina maswali kadhaa je wataarishaji Filamu kwa fursa hii ni
sisi tunapaswa kumtumia Ernest atupeleke katika levo za kimataifa
au Ernest atumie nafasi yake kutupeleka katika levo za kimataifa
kwa utaarishaji filamu ni fursa ambayo unaweza kusema imekuja
katika sahani ya dhahabu ,inakuwaje filamu nyingi zinazozungumzia
bara la Afrika hasa Afrika mashariki maeneo yanapotumika kupiga
picha hizo ni Kenya kwanini isiwe Tanzania!? kuna haja gani ya
kuwa na shirikisho la filamu Tanzania(TAFF), nini maana ya kuwa na
chama cha waigizaji Tanzania? umuhimu wa vyama hivi ni nini
hasa....!?