• Facebook
  • Twitter
  • Google Plus
  • Contact

FILM TANZANIA

FILM TANZANIA

  • Home
  • INTERVIEW
  • SIMULIZI
  • HABARI
  • BEHIND THE SCENES
  • LOCATION
  • ABOUT
    • Facebook
    • Twitter
    • Google Plus
Home » SIMULIZI » SAMAKI MTU(MERMAID) 05

SAMAKI MTU(MERMAID) 05

Add Comment
SIMULIZI



                                                       SAMAKI MTU(MERMAID)


                                                      SEHEMU YA TANO


 Simulizi :      SAMAKI MTU(MERMAID) 
 Mtunzi :         Jackson James .
Mawasiliano; +255 762 892 472:, +255 652 064 958
Email: jamesjacson0@gmail.com

 Millian alifika chuoni,mapema sana akiwahi ili akamalishe kazi ambazo alitakiwa azikamilishe muda wa wikiendi lakini alishindwa kifanya hivyo kutokana na kubwana na kazi nyingi za nyumbani katika siku hizo mbili za mapumziko,alijitahidi kufanya kazi hizo haraka ,wakati huo akimsubiri pia James awasili chuoni kutokana na kwamba hakupata nafasi ya kumuona siku nzima kutokana na ubize aliokuwa nao.zilianza sekunde,kisha dakika na baadae masaa yalipita bila james, kuonekana,alijaribu kupiga simu yake lakini ilikuwa haipatikani,hakupata jibu la haraka la kwanini James hakuwasili chuo bila kutoa taarifa lakini mbaya zaidi hata simu ilikuwa imefungwa,aliinuka haraka haraka na kwenda katika gari lake na kuliwasha kisha akaliondoa kwa kasi kuelekea kumuona James,kwani katika mawazo yake alijua kuna tatizo litakalokuwa limempata,mawazo hayo yalimfanya aongeze spidi ya gari Mara dufu Ili awahi kufika.
Akiwa anatoka katika Barabara ndogo ya kutoka chuoni kuingia katika makutano ya barabara kuu ya mji huku akiwa katika kasi ya ajabu,alitaharuki kuona gari nyingine ndogo ikiwa inakuja katika usawa wa gari yake upande wa kushoto kwake,alijikuta akiachia usukani na kufumba macho kwani asingeweza kuvumilia kuona kile kinachoenda kutokea,mwisho kilisikika kishindo kikubwa kilichofanya watu wengi waliona tukio hilo kuduwaa na kushika vichwa vyao.
********* **********
SAA 4:35 asubuhi ,ndio muda ambao ulioneshwa katika saa kubwa ya mezani iliyokuwa katika chumba cha James,wakati huo James alikuwa bado amelala huku akiwa amejikunyata katika blanketi kutokana na baridi Kali iliyokuwepo katika Siku hiyo,hakujali milio ya simu yake iliyokuwa ikiita Mara kwa mara saa moja lililopita,kwani alikuwa katika usingizi mzito kutokana na uchovu pamoja na kuwaza mambo ya ajabu aliyoyaona Jana kwa macho yake mwenyewe huko ufukweni,alijikuta akishituka baada ya muda mfupi na kuiangalia saa yake ya mezani iliyokuwa imewekwa pembeni mwa kitanda chake, ambayo muda huo ilionyesha ni saa 4:45 asubuhi “ nimechelewa kipindi chuoni”aliwaza ,kisha akaruka haraka haraka kutoka kitandani na kuelekea bafuni ili asafishe mwili wake ,aliporudi akajiandaa haraka haraka na kubeba vifaa vyake kuelekea 15

nje,alishuka ngazi za kutoka chumbani, haraka haraka na kufika sebuleni ,lakini alipotaka kufungua mlango wake wa kutokea nje ,akakumbuka amesahau simu kitandani,ilimbidi kuweka vifaa vyake pale chini na kurudi chumbani ,alifika akachukua simu lakini alipoangalia kuna simu nyingi amepigiwa na rafiki yake wa kike,aitwaye millian na kuna ujumbe alioutuma unasema “where are you ?,am coming to your place now”(upon wapi,nakuja nyumbani kwako sasa hivi,) alipojaribu kuangalia muda ujumbe ulipotumwa ni saa 2:57 asubuhi,lakini akiangalia muda wa sasa ni 5:02 adhuhuri,alibaki anajiuliza huku alishuka ngazi taratibu ,”mbona hakuja auamehairisha?”,”mbona hajapiga wala kuniandikia ujumbe kwamba amehairisha kuja”,hayo yote ni maswali ya haraka haraka yaliyokuwa yanapita katika akili yake kwa muda huo ,lakini hakuwa na majibu ya uhakika hivyo aliamua kumpigia Ili amfahamishe alipo,,lakini alipojaribu kutafuta namba ilikuwa haipatikani,alirudia Mara kwa Mara lakini majibu yalikuwa ni Yale jambo hili lilimpa wasiwasi,akashuka haraka haraka na kuchukua vifaa vyake ,na kuchukua gari yake ndogo, kuelekea chuoni ,alipofika karibu na makutano ya barabara kwa mbali aliona kuna gari ya kunyanyua na kubeba magari mabovu au yaliyoharibika ikihangaika kuyanyua magari madogo mawili yaliyokuwa yameharibika vibaya kutokana na kugongana katika eneo hilo,aliposogea katika eneo hilo kulikuwa na foleni ndogo iliyotokana na shughuli ya kutoa magari hayo iliyokuwa ikiendelea katika eneo hilo.James alipoona tukio lile ilimbidi ashuke kwenye gari na kwenda kuangilia kile kilichotokea ,haukutaka kuyaaminisha mawazo yake kwamba ajali ile inaweza kuwa imehusisha MTU wa karibu anaye mfahamu vizuri.Aliposogea karibu alisikia sauti za watu waliokuwa wakiongelea ajali ile wengi wakimuonea huruma sana msichana wa chuo cha northern Mariana university college,aliyekuwa katika gari ndogo ambayo iliharibika vibaya sana kutokana na kugongwa ubavuni kisha kupinduka na kubiringika Mara kadhaa kabla ya kurudi katika mkao wake, aliposogea mbele zaidi aliwaona wanachuo wenzake ,wakiwa wamekaa kivikundi vikundi katika hali ya majonzi na huzuni huku wengi wakiombea mungu aepushe mbali jambo baya linaloweza kutokea kwa mwenzao ambaye alikuwa katika hali mbaya sana kutokana na kuumia vibaya sehemu mbalimbali mwili wake,James alipokuwa anasogea upande walipokuwa wamesimama wanachuo wote waligeuka na kumtazama James kwa macho ya huruma wengine wakimuangalia kwa macho ya dharau , kwa mbali alisikia minon'gono iliyokuwa ikimshutumu yeye moja kwa moja kuhusika katika kusabahisha ajali hiyo iliyogharimu maisha ya msichana asiyekuwa na hatia .James hakujali mawazo yao juu yake alisogea na kumuuliza mmoja wa wanachuo wenzake walio kuwa pale,jibu alilopata lilimfanya aishiwe nguvu,miguu yake ilishikwa ganzi ghafla ,shati jepesi alilolavaa lilionekaana zito na alitamani alivue ,Alijikuta akiishiwa nguvu na alidondoka na kupoteza fahamu…..

0 Response to " SAMAKI MTU(MERMAID) 05"

← Newer Post Older Post → Home
Subscribe to: Post Comments (Atom)

FOLLOW US

POPULAR POSTS

  • KILA MWANDISHI WA MISWADA {SCRIPT}
    Kila mwandishi wa miswada {script} hutumia njia aipendayo kuitumia katika kuandika miswada {script}si kwa nchi yetu ya Tanzania pekee h...
  • IFAHAM HISTORIA YA KANUMBA YOTE KWA UJUMLA
    Hayati Steven Kanumba amezaliwa Januari 8 ,1984 Shinyanga,Tanzania Amefarki Aprili 7, 2012 (umri 28)Dar es Salaam,Tanzania Kaz...
  • SAMAKI MTU(MERMAID) 01
                                                                                                             SAMAKI MTU(MERMAID)   ...
  • MZEE MSISIRI ATUMBUA JIPU
    •••• ♦ •••• ♦ •••• ♦ •••• ♠ ••• ♦ 1. Jina langu kamili ni FADHILI RAJABU MSISILI 2. Kabira langu ni Chotara wa kizigua kwa baba na ...
  • SAMAKI MTU(MERMAID) 04
                                                                                                                          SAMAKI MTU(MERMAID...
  • ULINGO WA MOTO FILAM YA MAPIGANO YENYE UARISIA
    Daaah!!! Nikali tena ni noma sana,Usisa hau wala usikose kupata nakala yako.Tarehe 23/4/2018 filamu hii itakua tayari imo sokoni.....UL...
  • SAMAKI MTU(MERMAID) 02
                                                           SAMAKI MTU(MERMAID)                                                        ...
  • MFAHAM JUMA KILOWEKO SAJUKI
    Sajuki alizaliwa mwaka 1984, mkoani Songea na kupata elimu yake ya msing na sekondari hukohuko mkoani Songea.Ambapo mwaka 2005 aliweza ku...
  • JINSI YA KUTENGENEZA FILAM NA KUUZA
     KATIKA miongo kadhaa iliyopita filam nyingi zenye mafanikio zimetokezwa huko Hollywood. Hilo limekuwa na uvutano mkubwa ulimwenguni pote ...
  • SAMAKI MTU(MERMAID) 11
                                                                   SAMAKI MTU(MERMAID)                                                 ...
Back to top!
Copyright (c) 2014 FILM TANZANIA. All Rights Reserved Created by Flash TZ Blog. Designed by Flash TZ Blog. Powered by Blogger.