• Facebook
  • Twitter
  • Google Plus
  • Contact

FILM TANZANIA

FILM TANZANIA

  • Home
  • INTERVIEW
  • SIMULIZI
  • HABARI
  • BEHIND THE SCENES
  • LOCATION
  • ABOUT
    • Facebook
    • Twitter
    • Google Plus
Home » SIMULIZI » SAMAKI MTU(MERMAID) 10

SAMAKI MTU(MERMAID) 10

Add Comment
SIMULIZI




                                               
                                                    SAMAKI MTU(MERMAID)


                                                      SEHEMU YA KUMI


 Simulizi :      SAMAKI MTU(MERMAID) 
 Mtunzi :         Jackson James .
Mawasiliano; +255 762 892 472:, +255 652 064 958
Email: jamesjacson0@gmail.com       

James alikuwa amekaa katika chumba maalumu huku akiwa anaandaliwa na watu maaulumu waliokuwa wamewekwa kwaajili ya kazi hiyo ili kumfanya apendeze kabla ya kutoka nje ya chumba hicho na kuingia ukumbini kwaajili ya kulianza zoezi kubwa lililokuwa mbele yake ,hili ni zoezi la kumvalisha Pete ya uchumba Anna,ambae ni mchumba wake na ni msichana pekee aliyeko moyoni mwake tangu utotoni mwao.Akiwa amemaliza kuandaliwa na sasa akiwa amekaa kwenye kiti kikubwa kilichokuwa ndani ya chumba hicho huku akisubiri kuitwa au kufuatwa na wazazi wake katika chumba hicho kwaajili ya kuanza rasmi hafla hiyo ,alishangaa muda ukiwa unasogea na hakuna taarifa au mtu yoyote aliyekuja kumtaarifu juu ya kinachoendelea ,kwani muda uliokuwa umepangwa hafla kuanza,ulikuwa umeshapita ,Aliamua kunyanyuka mwenyewe Ili kutoka nje ya chumba hicho ,lakini alipofungua mlango tu ,alikutana na macho ya mr John ambae
27
ni baba wa Anna akiwa anajiandaa kuingia ndani ya chumba hicho pia ,huku akionekana mwenye haraka na uso wake ulijaa wasiwasi mwingi ,hali iliyomfanya James ashtuke na kuhisi lazima kuna jambo baya litakuwa limetokea,hvyo walirudi ndani wote na James alikaa kwenye kiti alichokuwa amekaa mwanzo ,lakini Mr john hakukaa alisimama tu japo kulikuwa na viti vingi ndani ya chumba hicho.
“whats going on Father “,(nini kinaendelea baba?),aliuliza james huku akiwa na hamu ya kujua kinachoendelea .
“Anna atakuwa amepatwa na tatizo ,kwa sababu tumejaribu kumtafuta kwenye simu haipokelewi,na pia hata ya dereva niliemtuma nae hapokei simu,sijui tatizo nini”,alisema mr john huku akihema na kushusha pumzi kwanguvu ,kuonyesha namna alivyo na wasiwasi mwingi juu ya mtoto wake.
“then(kwahiyo ),sasa mbona hatuendi kumfatilia huko aliko na mbona hamkunambia mapema,”aliuliza kwa hasirs james huku akianza kutetemeka mwili wake ,kutokana na mawazo na mshtuko uliompata baada ya kusikia taarifa hiyo ya kusikitisha ,ambayo pia imekuja wakati mbaya wakati ambao wawili hao walitarajiwa kuvishana pete ya uchumba.
“usijali james ,nimeshatoa taarifa polisi na wamesha nihakikishia kwamba hakuna ajali yoyote iliyolipotiwa siku hii ya Leo na wamenihaidi kufatilia swala hili na watanitaarifu kila watakachopata,lakini pia nimeshatuma vijana wangu watafute gari hiyo”,aliongea kwa msisitizo mr john huku akijikuna nywele zake zilizokuwa zimeanza kuota mnvi.
Baada ya kusikia maelezo Yale kutoka kwa mr john ,kidogo roho ya james ilianza kutulia japo bado alikuwa na wasiwasi wa wapi Anna alipo kwani hiyo ndio ilikuwa Mara yao ya kwanza kukumbwa na mkasa huo mkubwa zaidi katika maisha yao.
Mr john alijua namna kijana huyo atakavyokuwa ameshituka kwa kiasi kikubwa kutokana na taarifa hizo mbaya zilizokuwa zimekuja katika wakati ambao ulifaa kuwa wa furaha na amani kati yao hao,wawili.Aliondoka chumbani mle huku akimuacha James akiwa amejiinamia akiwa kama anasali kwa mungu mabaya yasimkute Anna,Lakini kabla hajafika mlangoni simu yake iliita na alipokea kwa haraka ,alikuwa ni mkuu wa upelelezi wa Polisi katika jiji hilo,ambae pia ni rafiki wa karibu wa mr John ,akimtaarifu juu ya kupatikana kwa gari yake pamoja na watu wawili waliokuwa wamefungwa kamba na kupuliziwa madawa ya usingizi,ambapo hadi sasa wamekimbizwa katika hospitali kubwa iliyopo katika jiji hilo.Taarifa hizi zilimshtua sana na hakutaka kuuliza zaidi alikata simu na kutoka kwa kasi kwenda nje ,huku akimuacha James akiwa anamshangaa lakini na yeye alitoka nyuma na kumfata alikoenda.
************** ***********.
28
Wazazi wake na millian walionekana wakiwa na furaha mbele ya nyuso zao lakini pia walikuwa na mioyo iliyobeba huzuni na huruma nyingi juu ya binti yao ,ambae japo alikuwa amepata nafuu na kurejewa na fahamu zake zaidi ya Siku mbili sasa,bado alikuwa amelala kitandani huku akiendelea kufanyiwa uchunguzi wa Mara kwa Mara na madaktari.Ni zaidi ya miezi miwili sasa milian amewafanya wazazi wake hao kushindwa kuendelea na majukumu yao ya kila siku na kubaki kuwa karibu naye Ili kumuuguza na kumfariji hospitalini hapo.
Jambo kubwa lililowaumiza vichwa wawili hao ni kitendo cha millian ,mara baada ya kurejewa na fahamu na kuamka ,swali la kwanza kwake ni kuuliza wapi alipo james ,ambae mpaka sasa hawajui ninani? Na anaumuhimu gani maishani mwake mpaka amfanye ashindwe kufikiria namna wao walivyohangaika kwaajili yake tangu alipopata ajali ,namna walivyokuwa hawapati usingizi wala kupumzika kwaajili yake,lakini mwisho wa siku anamtaja mtu ambae hawajawahi kumuona tangu binti yao huyo apate ajali.
Suala hili lilikuwa likizidi kuisumbua akili ya mr Richard kila Mara na alililazimika kwenda kumuuliza binti yake juu ya suala hili kwani inawezekana kijana huyo ndie huyo anayemtafta kwa kuhisiwa ndo sababu kuu ya binti yake kupata ajali mbaya iliyomfanya alale kitandani kwa muda wa miezi miwili sasa na zaidi sasa.
Aliingia chumbani alipolazwa millian na hakumkuta mke wake ambae pia ni mama yake na millian,ndani ya chumba hicho , millian alionekana amefumba macho lakini akiwa hajasinzia katika muda huo wa adhuhuri,kwani mr Richard alipofungua mlango kwaajili ya kuingia ndani ya chumba hicho,aliweza kumuona na akamuita .
“dad(baba),aliita millian ..
“Ooh sorry my daughter ,are you tired now?”,(ooh samahani binti yangu ,vipi umechoka sasa,?),aliuliza mr Richard huku akisogea mahali alipokuwa amelala binti yake na kisha kukaa pembeni yake.
“Don’t worry much about me father, am ok,but it seems you are not feeling well,are you fine?”,(usijali kuhusu mimi baba ,nipo sawa,lakini unaonekana haupo sawa vipi mzima?),aliuliza millian baada ya kugundua baba yake hayuko sawa ,kwani hata uso wake ulionyesha hivyo.
“No am fine ,but am just worry about you”(hapana nipo sahihi ,ila nawaza kuhusu wewe),alijibu mr Richard huku akishika mkono wa binti yake na kuufuta futa na kitambaa kilichokuwa pembeni yake.
“thank you dad,am very proud to have father like you “(asante baba ,nina jivunia kuwa na baba kama wewe)alijibu millian huku akitabasamu.
29
“Millian ,I just want to know who is james to you,is he the one who made you to be like this today?,”(millian,nataka kujua tu James ninani kwako ,je ni yeye aliyekufanya kuwa kama hivi leo”,aliuliza kwa hasira mr Richard huku akiyauma meno yake ,hali ambayo millian pia aliitambua na alijua baba yake tayari anahasira ambazo huweza kumfanya kufanya kitu chochote kibaya kwa mtu ambae atacheza na familia yake jambo ambalo millian hakutaka litokee kwa james .Alikaa kimya kwa muda ili kufikiri jibu sahihi litakalomuokoa james katika janga hilo ,mwishowe akalipata akilini mwake kabla ya kufungua mdomo wake na kujibu……
********* **********

0 Response to "SAMAKI MTU(MERMAID) 10"

← Newer Post Older Post → Home
Subscribe to: Post Comments (Atom)

FOLLOW US

POPULAR POSTS

  • KILA MWANDISHI WA MISWADA {SCRIPT}
    Kila mwandishi wa miswada {script} hutumia njia aipendayo kuitumia katika kuandika miswada {script}si kwa nchi yetu ya Tanzania pekee h...
  • IFAHAM HISTORIA YA KANUMBA YOTE KWA UJUMLA
    Hayati Steven Kanumba amezaliwa Januari 8 ,1984 Shinyanga,Tanzania Amefarki Aprili 7, 2012 (umri 28)Dar es Salaam,Tanzania Kaz...
  • SAMAKI MTU(MERMAID) 01
                                                                                                             SAMAKI MTU(MERMAID)   ...
  • MZEE MSISIRI ATUMBUA JIPU
    •••• ♦ •••• ♦ •••• ♦ •••• ♠ ••• ♦ 1. Jina langu kamili ni FADHILI RAJABU MSISILI 2. Kabira langu ni Chotara wa kizigua kwa baba na ...
  • SAMAKI MTU(MERMAID) 04
                                                                                                                          SAMAKI MTU(MERMAID...
  • ULINGO WA MOTO FILAM YA MAPIGANO YENYE UARISIA
    Daaah!!! Nikali tena ni noma sana,Usisa hau wala usikose kupata nakala yako.Tarehe 23/4/2018 filamu hii itakua tayari imo sokoni.....UL...
  • SAMAKI MTU(MERMAID) 02
                                                           SAMAKI MTU(MERMAID)                                                        ...
  • MFAHAM JUMA KILOWEKO SAJUKI
    Sajuki alizaliwa mwaka 1984, mkoani Songea na kupata elimu yake ya msing na sekondari hukohuko mkoani Songea.Ambapo mwaka 2005 aliweza ku...
  • JINSI YA KUTENGENEZA FILAM NA KUUZA
     KATIKA miongo kadhaa iliyopita filam nyingi zenye mafanikio zimetokezwa huko Hollywood. Hilo limekuwa na uvutano mkubwa ulimwenguni pote ...
  • SAMAKI MTU(MERMAID) 11
                                                                   SAMAKI MTU(MERMAID)                                                 ...
Back to top!
Copyright (c) 2014 FILM TANZANIA. All Rights Reserved Created by Flash TZ Blog. Designed by Flash TZ Blog. Powered by Blogger.