SAMAKI MTU(MERMAID)
SEHEMU YA TISA
Simulizi : SAMAKI MTU(MERMAID)
Mtunzi : Jackson James .
Mawasiliano; +255 762 892 472:, +255 652 064 958
Email: jamesjacson0@gmail.com
Anna alichelewa kuamka Siku hiyo kutokana uchovu aliokuwa nao mwilini uliomfanya ashindwe kutambua kwamba muda wa kuamka ulikuwa umeshafika,aliendelea kulala huku akibembelezwa na ubaridi wa mbali uliokuwepo siku hiyo.Ilipotimia SAA 5,asubuhi saa yake ya mezani ilipiga kengele iliyokuwa inalenga kumkumbusha mmliki wake kwamba ni muda wa kupata kifungua kinywa ,Kengele ile ilipenya vyema masikioni mwa Anna lakini bado alikuwa mbishi wa kunyanyuka na kubaki akijigeuza huku na huko Ili kukwepa sauti ya kengele hiyo iliyokuwa ikilia kwa nguvu na kufanya ukimya wakutisha ndani ya nyumba ile kila ilipokuwa ikitulia kabla ya kurudia tena na tena.Mwishowe Anna ilimbidi kutii amri ya kengele hiyo aliyokuwa ameiweka mwenyewe ,alitupa shuka lake zito pembeni na kufumbua macho yake taratibu huku akijinyosha huku na huko,yeye mwenyewe hakutaraji muda ungekuwa umeenda kiasi hicho na hakutaka kuamini kabisa kwamba muda alioamka ni SAA tano,Alijinyosha tena kwa nguvu na kushusha mikono yake taratibu,kisha alisogea mwishoni mwa kitanda na kuishusha miguu yake chini ya zulia safi lililokuwa chini ya kitanda chake.
Aliamua kwenda kufanya usafi wa mwili wake kabla ya kufanya usafi wa ndani ya nyumba yake na kuandaa kifungua kinywa kwani muda ulikuwa umeenda sana na alikuwa hajafanya jambo lolote.Akiwa anapiga hatua kwenda Bafuni ,alisikia simu yake ya mkononi ikiita na aliamua kurudi kwenda kuipokea ,aliangalia kwenye kioo cha simu yake hakukuta jina la mpigaji wa simu hiyo ila namba ilionyesha mpigaji wa simu hiyo anatoka nje ya nchi.
“Hallow,”aliongea Anna kwa upole.
“hallow anna mzima mwanangu”,ilikuwa ni sauti ya mr John ,baba yake mzazi na Anna sauti ambayo Anna aliitambua vyema .
24
“Aaah dad (baba)shikamoo,mbona umetumia namba nyingine,umeniogopesha sana “ ,aliongea Anna huku akitabasamu.
“ hahahaa…pole mwanangu sikutegemea nitakushitua kiasi hicho”,aliongea mr john, huku akicheka sana.
“Usijali baba “,aliongea Ana kwa aibu.
“Wiki ijayo kutakuwa na jambo muhimu tuliloliandaa kwaajili yako,naomba ujiandae “,aliongea kwa kusisitiza mr john,hali iliyomfanya Anna atamani kujua nini kimeandaliwa kwaajili yake.
“kitu gani baba?”,aliuliza Anna kwa hamu kubwa.
“Usijali nakuja huko wikiendi hii ,nitakutaarifu zaidi “,alijibu Mr john huku akimuhakikishia binti yake ujio wake.
“Sawa dad(baba ),asante”,alijibu Anna huku akirusha rusha miguu yake chini.
Anna alifurahia Ujumbe huo aliopewa na baba yake japo hakujua ni Ujumbe wa nini nanikitu gani muhimu wazazi wake walikuwa wameandaa kwaajili yake katika siku hiyo mpaka waitenge kuwa siku maalumu inayowafanya wasafiri kutoka Tanzania kuja Marekani,aliwaza sana lakini hakupata majibu kwani hajawaho kufanyiwa jambo kubwa kama hilo kabla ,mwishowe aliamka na kuvaa viatu vyake vya kukanyagia tayari kwa kuelekea bafuni kufanya usafi wa mwili wake,huku akizidi kuumiza kichwa kama ataweza kutambua umuhimu wa siku hiyo kwake na kwa wazazi wake.
*************** ***************
Mama yake na millian aliingia katika chumba alicholazwa mwanae akiwa amebeba vifaa vya kumsaidia katika kusafisha mwili wa mwanae ambae muda wote alikuwa amelala huku viungo vyake vyote vya mwili vikiwa vimetulia ,isipokuwa moyo wake ambao mapigo yake yaliyokuwa yamebeba matumaini pekee ya binti huyo mdogo ,ambae bado alihitaji kupumua japo aweze kutimiza mambo mengi yakiwemo malengo mbalimbali aliyojiwekea maishani mwake ambayo yote kwa pamoja yalihitaji uhai wake Ili yaweze kutimizwa.
Si kwamba madaktri naii manesi Wa hospitali ya apolo hawakufanya jitihada katika kuhakikisha Millian,anarejewa na fahamu zake,walijitahidi kwa kila kitu na walitumia njia nyingi katika kuhakikisha binti huyo anapata fahamu na kurejea katika Hali yake ya kawaida ,kwani hata vipimo vyote vilivyofanyika vilionesha kwamba hakuna tatizo lingine alilokuwa nalo millian ,zaidi ya majeraha madogo madogo aliyoyapata wakati wa ajali,majeraha ambayo yalikuwa yameisha tibiwa yote na mengine yalikuwa yameanza kujifuta kabisa katika kipindi hicho cha miezi miwili lakini hali ya millian kuendelea kulala na kutopata fahamu ni jambo ambalo liliwashangaza wengi.
25
Mama millian,akiwa anaendelea kumfuta mwanae na kitambaa cha maji safi ,alikuwa pia akimuangalia mwanae huyo kwa huzuni kwani hakutarajia maisha ya mwanae yaitaishia kitandani namna hiyo,kila alipokumbuka tabasamu la mwanae ,sauti ya mwanae,na vituko mbalimbali alivyokuwa akivifanya mwanae pindi akiwa nyumbani ,chozi la huruma halikuzuilika kumtoka kutokana na machungu na mapenzi ya dhati aliyonayo juu mwanae,
“Mom”(mama),ilikuwa nisauti iliyosikika chumbani mule ikimuita mama yake na millian, ambae kwa muda huo alikuwa ameupa uso wa binti yake mgongo ,huku akiifuta taratibu miguu ya mwanae,ni kweli kwamba mama huyu aliisikia vyema sauti hiyo ya mwanae lakini hakuwa tayari kutaka kuamini kwamba sauti hiyo ni ya millian,hivyo aliamini sauti ile inasikika kwaaajili ya mawazo mengi aliyonayo juu ya mtoto wake.
“mom”(mama),sasa hivi sauti iliita kwa nguvu zaidi na kupenya vyema kwenye masikio ya mama yake na millian ambae aligeuka kwa haraka ,na kumuangalia millian ambae kwa mara ya kwanza tangu apate ajali fahamu zake zinarejea na anafumbua mdomo wake huku akiyapiga piga macho yake kama mtu aliyetazama mwanga wa jua kwa muda .
**************** ************
Tarehe 10/8/2003 , ndio siku pekee iliyokuwa imepangwa kwaajili ya hafla fupi iliyokuwa imeandaliwa na mr David ambae pia ni baba wa kijana james,na pia ni mwenyekiti wa kampuni kubwa na maarufu jijini new York,naizungumzia J.D,company limited,.Siku hii ilikuwa imetengwa maalumu kwaajili ya mwenyekiti huyu kumtangaza mrithi wa kampuni hiyo ambae ni mwanae wa pekee ,ambae ni James,lakini pia ikitarijiwa kushuhudiwa kijana huyu akimvisha Pete ya uchumba mpenzi wake wa siku nyingi ambae walilelewa nae pamoja tangu utotoni,Hapa namzungumzia Anna.
Hadi kufikia muda wa saa 3 asubuhi,watu karibia wote waliokuwa wamealikwa katika hafla hiyo walikuwa wamekwishafika,miongoni mwao wakiwemo matajiri maarufu jijini new York na nje ya jiji hilo kubwa,wote walikuwa wakiendelea kuburudika na muziki wa taratibu uliokuwa ukiendelea kuburudisha ,huku wakipata vinywaji na vyakula mbalimbali walivyokuwa wakiviagiza kutoka kwa wahudumu waliokuwepo katika ukumbi huo mkubwa.Wazazi wa Anna ambao pia walikuwa wamesafiri kutoka Tanzania kuja nchini Marekani kwaajili ya kushiriki kwa pamoja na familia rafiki ya mr David katika hafla ,,walikuwa katika chumba maalumu katika ukumbi huo wakiendelea kujiandaa kwaajili ya kuingia ukumbini huku wakiwa wanaambatana na mtoto wao Huyo ambae kwa muda huo alikuwa hajafika ,japo walikuwa na matumaini ya yeye kufika muda wowote kutokana na ahadi aliyokuwa amewapatia Anna ya kufika ukumbini hapo dakika chache zijazo kwani alikuwa anamalizia kujiandaa ,jambo lililomfanya mr john kumuagiza dereva wake achukue gari yake na kumfata binti Huyo Ili awahi ukumbini kwani muda wa kuanza ulikuwa umekaribia kufika.Lakini cha kushangaza dakika zilizidi kwenda na hakukuwa na MTU yoyote aliyeingia ukumbini hapo,Mr john alipojaribu kutafuta simu ya Anna ,iliita bila kupokelewa ,vivyo hivyo
26
alipompigia dereva wake aliyemtuma kumfata Anna pia simu yake ilikuwa haipatikani,hali hii ilimpa wasiwasi sana kwani alihisi kuna jambo baya litakuwa limetokea kwa watu hawa wawili.
**************** ***************
Anna alipomaliza kujiandaa ,alienda kwenye meza yake ya mapambo kujiangalia na kuona kama atakuwa amependeza vya kutosha ukizingatia Leo ndio siku aliyokuwa akiisubiri zaidi maishani mwake yeye na james , ambapo ni katika kipindi cha miaka kumi na sita sasa imepita, tangu walipowekeana ahadi ya kuja kuoana pindi watakapokuwa wakubwa ahadi ambayo katika siku hii ya Leo itakuwa ikipiga hatua kuelekea kutimia .Anna alikuwa na furaha kubwa zaidi moyoni mwake kwani hakuamini kwamba IPO siku wataweza kutimiza ahadi hiyo ambayo Mara nyingi huwashinda watu wengi kutokana na vishawishi vingi vilivyopo duniani.
Alipokamilisha kujipamba na kujiona katika kioo kikubwa kikichopo chumbani kwake ,alichukua pochi yake ndogo iliyokuwa na ranging nyekundu,rangi iliyoendana vyema na nguo alizozivaa ,alipiga hatua za haraka na kutoka nje ya nyumba yake ,alipokwisha kurudishia mlango wa nyumba yake ,aliona gari ndogo ya kifahari aina ya misd Benz, yenye vioo vyeusi, iliyokuwa imepaki nje ya geti la nyumba yake,na alitabasamu alipoitambua gari ile kuwa ni ya baba yake kutokana na kuona nembo ndogo ya kampuni ya baba yake ,pembeni ya mlango wa mbele .Anna alijua baba yake atakuwa yupo ndani ya gari hiyo na atakuwa amechukia kitendo cha yeye kuchelewa .Alirudishia geti lake kisha akapiga hatua za haraka na kuufata mlango wa gari hiyo na akafungua na kupanda kwa haraka kisha akaufunga kwa nguvu,gari ikaondolewa kwa kasi,lakini alihisi jambo lisilo la kawaida kwani alikuta kuna kuna MTU tofauti na baba yake akiwa ndie anaendesha gari hiyo ,mbaya zaidi alikuwa amefunika sura yake kwa kitambaa cheusi,hapo kengele ya hatari ikalia akilini kwa Anna ,lakini alikuwa ameshachelewa kwani na yeye pia alibanwa pua na mdomo kwa kitambaa maalumu chenye dawa ,MTU aliyefanya hivy hakuweza kumuona kwani alikuwa nyuma ya siti yake .Macho yake yaliishiwa nguvu na kuingia Giza la ghafla ,mwishowe alishindwa kutambua kilichokuwa kikiendelea katika muda huo.