• Facebook
  • Twitter
  • Google Plus
  • Contact

FILM TANZANIA

FILM TANZANIA

  • Home
  • INTERVIEW
  • SIMULIZI
  • HABARI
  • BEHIND THE SCENES
  • LOCATION
  • ABOUT
    • Facebook
    • Twitter
    • Google Plus
Home » SIMULIZI » SAMAKI MTU(MERMAID) 08

SAMAKI MTU(MERMAID) 08

Add Comment
SIMULIZI

                                    
                                                       SAMAKI MTU(MERMAID)


                                                      SEHEMU YA  NANE


 Simulizi :      SAMAKI MTU(MERMAID) 
 Mtunzi :         Jackson James .
Mawasiliano; +255 762 892 472:, +255 652 064 958
Email: jamesjacson0@gmail.com        



Siku ya tarehe 28/7/2003
,vyuo vingi vya serikali vilikuwa vimefungwa hii nikutokana na kupisha muda wa miezi miwili ya likizo kwa wanachuo ikiyokuwa imetengwa na serikali ya marekani.
Katika uwanja wa ndege wa spain international airport ,James alikuwa akijiandaa kuondoka Mariana kuelekea new York ilipo familia yakeAlikuwa amesindikizwa na rafiki yake wa karibu ambaye amekuwa akimsaidia Mara kwa Mara tangu alipokuwa amelazwa hospitalini kwa sababu ya kupoteza fahamu.
“hey bye “(hoya kwaheri)alikuwa ni joasi akimuaga james huku akimpa mkono wa kumtakia heri katika safari yake hiyo.
“bye too man,take care for your own”(kwaheri pia ,jiangalie wewe mwenyewe)alisema james huku akivuta begi lake kuingia ndani ya uwanja wa ndege,joasi alibaki akiwa anampungia mkono na akimsindikiza kwa maneno ya faraja yaliyojaa matumaini na salamu nyingi huko aendako.
Baada ya masaa 2 ,ndege kubwa ya abiria ilikuwa ikitua katika uwanja wa ndege John f.Kennedy international aiport.,James alishuka taratibu kwenye ndege na kuelekea mahali pa kupumzikia abiria . Lakini akiwa anapiga hatua fupi kuelekea eneo hilo alikuja mwanamme mmoja aliyekuwa amevaa suti na miwani myeusi ,mtu huyu aliyekuwa na asili ya kiafrika ni msaidizi Mkuu wa tajiri maarufu katika jiji la newyork na baba wa kijana james,.
“habari nimetumwa nije kukupokea” aliongea msaidizi yule huku akimpa mkono james .
“asante”alijibu james huku akimpa mizigo msaidizi yule ambaye aliibeba vizuri na kuelekea kwenye gari aliyokuja nayo uwanjani hapo.
“Oooh karibu sana james”ilikuwa ni sauti ya mama yake na james ikimkaribisha mwanae ambaye alikuwa akipanda ngazi za kuingia kwao taratibu,
“Asante mama “alijibu james huku akiwa anatabasamu na kumkumbatia mama yake baada ya kukutana nae mlangoni.
Ilikuwa ni siku ya furaha kwa familia hiyo ambayo ilikuwa ikimkaribisha mtoto wao wa pekee ambae alikuwa mbali nao kwa muda mrefu.Hata Mr david mbali na kutuma mtu wa kumpokea mtoto wake bado aliwahi kutoka mapema kazini kwake na kuja kujiunga na familia yake siku hiyo.
************ ************
Katika hospitali ya appolo nchini India alipolazwa millian kwaajili ya kupata matibabu ,madaktari bingwa wa hospitali hiyo wakiwa wamekusanyika katika chumba maalumu cha uchunguzi ,wakijitahidi kuyatetea maisha ya milliani ambae Leo alikuwa akikamilisha miezi miwili bila kupata fahamu zake.Wazazi wa binti huyu walikuwa wakiwaza na kuwazua hali aliyonayo mtoto wao ,hali ambayo ilikuwa ikizidi kubadilika siku hadi siku.
“She will recovery very soon don’t worry much”(atapona mapema sana ,usiwe na wasiwasi juu ya hilo),alikuwa ni daktari mmoja aliyetoka nje ya chumba alicholazwa Millian na kuja 22

kuwaona wazazi wa binti huyo waliokuwa wamekaa nje ya chumba hicho na wasi wasi mwingi ukijionesha dhahiri katika nyuso zao .
“ooh doctor thank you for your hard work”,(ahha dakitari asante kwa kazi yenu ngumu),alijibu Mr Richard huku akiwa ameshika kiuno chake ,na kutweta kwa nguvu kama mtu aliyekuwa anakimbizwa na mnyama mkali .Madakitari walipokamilisha zoezi lao walilokuwa wakilifanya walitoka nje na kuwaruhusu wazazi wa Millian kuingia ndani ya chumba hicho kumuona mtoto wao,Aliingia kwanza mama yake na millian ,lakini Mr Richard ambae ndo baba wa millian alishindwa kuingia kwenye chumba hicho na alibaki mlangoni akiangalia kwa mbali namna mke wake alivyokuwa akimuangalia mtoto wao Huyo kwa huruma huku machozi yakimtiririka machoni kama maji ,kiukweli uvumilivu ulimshinda na alitoka na kwenda nje ya hospitali hiyo na kwenda kupumzika kwenye bustani iliyokuwa nje ya majengo ya hospitali hiyo kubwa.
*********** ***********
Siku ya jumamosi,Asubuhi na mapema james aliamka na kuanza kuzunguka zunguka kwenye Bustani nzuri ya maua iliyokuwa nje ya nyumba yao, Ni muda mrefu sana umepita hakuwahi kupata nafasi ya kufanya hivyo kutokana na kuwa masomoni kwa muda wa miaka mitatu sasa na hatimae Leo anapata nafasi ya kufurahia harufu nzuri ya maua iliyokuwa ikipatikana eneo hilo pekee.Eneo lile pia lilimkumbusha miaka ya nyuma alipokuwa mdogo ,alikuwa na msichana waliependana sana na waliesaidiana kwa mambo mengi utotoni,Walipenda sana kucheza eneo hilo huku wakizunguka na kujificha katika maua madogo madogo yaliyokuwa yameshikamana na kutengeneza kitu kama vichaka vidogo ambavyo walivitumumia kujificha na kuzunguka zunguka,James alijikuta akitabasamu alipoyafikiria hayo yote akilini mwake.Akiwa anaendelea kushangaa na kutembelea maeneo mbalimbali ya Bustani hiyo,alishtushwa na sauti ya baba yake iliyotokea upande wa nyuma.
“James ,mbona mapema sana huku?”,alikuwa ni baba yake akimuuliza .
,”ooh nipo naangalia angalia Maya haya”,alijibu james huku akigeuka na kumuangalia babs yake.
“inaonekana unayapenda sana?”,aliuliza Mr David huku akipiga miayo mikali kwa uchovu aliokuwa nao kutokana na kwamba alikuwa ndo anatoka kuamka ,jambo lililomfanya james atabasamu.
“Ndio dad(baba),nayapenda sana na yananikumbusha mbali “,alijibu james huku akisogea na kumtoa mdudu aliyekuwa ametua begani kwa baba yake..
“asante,ushapata mchumba James?”,aliuliza Mr David huku akitabasamu.
“Hapana baba bado sijaamua ni nani wa kuwa nae maishani mwangu lakini pia masomo yamenibana”, alijibu james huku akimuangalia baba yake usoni.
“Unamkumbuka Anna”,aliuliza Mr David .
“Yeah si yule mtoto wa Mr John”,alijibu kwa kujiamini James lakini akiwa ana uhakika wa jibu lake.
“ndio,kumbe unamkumbuka ,huyo ndie MTU unayepaswa kumuoa kwa sababu mnafahamiana vizuri zaidi na ni mtoto mwenye heshima “,aliongea kwa msisitizo Mr David huku akimpiga piga James mabegani kwake. 23

“aahha ,sawa baba lakini Yuko wapi”,aliuliza James huku akionyesha kusubiri jibu la baba yake kwa hamu.
“ yupo hapa marekani na muda ukifika utamuona lakini siku hiyo pia itakuwa ni siku ya nyie wawili kuvishana Pete za uchumba.”,aliongeza Mr David huku akitabasamu.
“Siku gani hiyo baba”,aliuliza tena james
“wiki ijayo baada ya wazazi wa Anna kufika hapa Marekani” ,alijibu Mr David huku akianza safari ya kuekekea ndani .
“…ok(sawa)…”,alijibu james kwa kusitasita.
Mr david alishangazwa na hali aliyoionesha James ,baada ya kuambiwa swala la kumuoa Anna kwani hakuonesha kushtuka wala kupinga suala hilo ,jambo hill lilimfanya mr David atambue mapenzi ya dhati aliyonayo mtoto wake kwa binti huyo

0 Response to "SAMAKI MTU(MERMAID) 08"

← Newer Post Older Post → Home
Subscribe to: Post Comments (Atom)

FOLLOW US

POPULAR POSTS

  • KILA MWANDISHI WA MISWADA {SCRIPT}
    Kila mwandishi wa miswada {script} hutumia njia aipendayo kuitumia katika kuandika miswada {script}si kwa nchi yetu ya Tanzania pekee h...
  • IFAHAM HISTORIA YA KANUMBA YOTE KWA UJUMLA
    Hayati Steven Kanumba amezaliwa Januari 8 ,1984 Shinyanga,Tanzania Amefarki Aprili 7, 2012 (umri 28)Dar es Salaam,Tanzania Kaz...
  • SAMAKI MTU(MERMAID) 01
                                                                                                             SAMAKI MTU(MERMAID)   ...
  • MZEE MSISIRI ATUMBUA JIPU
    •••• ♦ •••• ♦ •••• ♦ •••• ♠ ••• ♦ 1. Jina langu kamili ni FADHILI RAJABU MSISILI 2. Kabira langu ni Chotara wa kizigua kwa baba na ...
  • SAMAKI MTU(MERMAID) 04
                                                                                                                          SAMAKI MTU(MERMAID...
  • ULINGO WA MOTO FILAM YA MAPIGANO YENYE UARISIA
    Daaah!!! Nikali tena ni noma sana,Usisa hau wala usikose kupata nakala yako.Tarehe 23/4/2018 filamu hii itakua tayari imo sokoni.....UL...
  • SAMAKI MTU(MERMAID) 02
                                                           SAMAKI MTU(MERMAID)                                                        ...
  • MFAHAM JUMA KILOWEKO SAJUKI
    Sajuki alizaliwa mwaka 1984, mkoani Songea na kupata elimu yake ya msing na sekondari hukohuko mkoani Songea.Ambapo mwaka 2005 aliweza ku...
  • JINSI YA KUTENGENEZA FILAM NA KUUZA
     KATIKA miongo kadhaa iliyopita filam nyingi zenye mafanikio zimetokezwa huko Hollywood. Hilo limekuwa na uvutano mkubwa ulimwenguni pote ...
  • SAMAKI MTU(MERMAID) 11
                                                                   SAMAKI MTU(MERMAID)                                                 ...
Back to top!
Copyright (c) 2014 FILM TANZANIA. All Rights Reserved Created by Flash TZ Blog. Designed by Flash TZ Blog. Powered by Blogger.