Filamu (kutoka Kiing. Movie au Motion pictures) ni mfululizo wa picha zinazoonyesha mwendo wa watu au vitu na kuonekana mbele ya watazamaji kwenye skrini. Ni aina ya mawasiliano yanayotumiwa kutolea hadithi au kuwaelezea watu kuhusiana na kujiofunza fikra au mitazamo mipya katika jamii. Watu katika kila pembe ya dunia huwa wanaangalia filamu ambazo zinaelezea hadithi fulani ikiwa kama kiburudisho, au njia ya moja wapo ya upenzi. Filamu nyingi zinatengenezwa zikiwa zinategemewa kuonyeshwa katika makumbi makubwa ya video au masinema.
Misingi ya kuona mwendo kwa njia ya filamu
Msingi wa filamu ni mbinu wa kushika mwendo fulani kwa picha nyingi. Kila picha pekee yake inaonyesha tu hali fulani bila mwendo. Lakini jicho la kibinadamu likiona picha zaidi ya 15 kwa sekunde haiwezi tena kuona tofauti kati ya picha hizi moja-moja inaanza kuona mwendo mfululizo. Kwa hiyo lazima kuwa na kamera inayopiga angalau picha 15 au zaidi kwa sekunde kupata filamu itakayoonekana kama mwendo halisi. Idadi ya picha 24 kwa sekunde ilikuwa wastani ya kawaida kwa muda mrefu.
Filamu za kwanza zilikuwa bila sauti lakini kuanzia miaka ya 1920 teknolojia ya kuwa na sauti pamoja na picha ilianza kupatikana.
Filamu za kuchorwa zilitumia misingi ileile yaani wachoraji walipaswa kugawa mwendo katika picha mfululizo zilizopigwa pcicha moja-moja na kuonyeshwa mfululizo.
Siku hizi sehemu kubwa za filamu hutengenezwa kwa kompyuta.
Filamu namna inavyotengenezwa
Mwandikaji muswaada andishi (screenwriter), anaandika muswaada huo utakao tumika katika filamu na waigizaji watafuata muswaada huo. Kisha mtayarishaji anakodisha watu watakaoshiriki na kutafuta pesa zote zitakazohitajika kuwalipa waigizaji na vyombo vya utenegezaji wa filamu.
Mtayarishaji mara nyingi hupata hela za kufanyia kazi hiyo kwa kupitia mikopo ya benki au wawekezaji watakao msaidia kumkopesha fedha kwa ajili ya matayarisho ya filamu hiyo. Kuna baadhi ya watayarishaji wanafanya kazi katika mastudio ya utengenezaji wa filamu, na kuna wengine hujitegemea (hawafanyikazi katika mastudio ya utayarishaji wa filamu).
Waongozaji na waigizaji husoma muswaada andishi ili kufahamu ni nini cha kusema na ni nini cha kufanya. Waigizaji wanahufadhi maneno ambayo watakayosema wakati wa kuigiza filamu, na kujifunza matendo ambayo muswaada andishi ulivyowaeleza vya kufanya. Kisha mwongozaji anaanza kuwaambia waigizaji nini cha kufanya na kumruhusu mpiga picha aanze kufnya vitu vyake kwa kutumia kamera ya kutengenezea filamu.
Mhariri wa filamu anaviunganisha vipande vya picha pamoja, na kuanza kuchagua vipande vitakavyofaa kwa wapenzi wa filamu. Mhandisi wa sauti na wataalamu wa kutengeneza vibwagizo vya filamu, hukusanyika pamoja na kuanza kuweka milio maalum katika filamu hiyo.
Pindi filamu inapokamilikae, nakala nyingi za filamu hutengenezwa na kusambazwa kupitia katika mikanda maalum kuhifadhia filamu na kuanza kuisambaza katika majumba ya sinema kwa ajili ya kuizindua na kisha baadaye kuipeleka mauzoni.