SAMAKI MTU(MERMAID)
SEHEMU YA SABA
Simulizi : SAMAKI MTU(MERMAID)
Mtunzi : Jackson James .
Mawasiliano; +255 762 892 472:, +255 652 064 958
Email: jamesjacson0@gmail.com
Baridi iliyokuwepo katika visiwa vya Mariana asubuhi ile ,Ilipenya matundu ya hewa yaliyowekwa moja ya vyumba katika hospitali ya ndogo ya genesis,mahali alipolazwa James ambae ni siku mbili zimepita tangu apate fahamu ,lakini hakuruhusiws kuondoka hospitalini pale kwani hali yake ilikuwa bado si nzuri kutokana na kupata mshituko moyoni mwake hasa alipoambiiwa kuwa ni millian ndiye alipata ajali mbaya .Alifungua macho taratibu na kuangaza huku na huko chumbani kwake lakini hakuona MTU yoyote,macho yake bado yalikuwa ni mazito na yenye ukungu ,kuashiria bado alikuwa na usingizi wa kutosha. “are you wake up now”(umeamka sasa),ilikuwa ni sauti ya joasi ,mtu pekee ambae amekuwa akikaa na kumuuguza james ,tangu alipopatwa na tatizo, “yeah ,are you fine”(ndiyo ,wewe hujambo?)alijibu james huku akijitahidi kujigeuza upande alipokuwa rafiki yake huyo mwenye asili ya kizungu . “yeah am good ,ooh I think today you will be discharged”(ndio sijambo,nadhani Leo utakuwa ukiruhusiwa kutoka ?),alisema joas ,”ooh real,?’”(aahh! Kweli)james aliuliza kwa mshangao
uliosindikizwa na furaha iliyojionesha wazi usoni kwake, “yeah”(ndio),alijibu joas huku akimsaidia James kuinuka kitandani .”thank you joas “(asante joas),alishukuru james kwa msaada na upendo aliouonyesha joasi,” ooh ,I didn’t do that much you know”(aah sijafanya ,mambo mengi unajua”)alijibu joas huku akimpiga piga james begani. Walikaa wakipiga story za hapa na pale lakini pia james alipewa habari na joas ,kwamba millian amehamishwa hospitali na amepelekwa India kwa matibabu zadi ,roho ilimuuma sana james kwani alijutia kila kitu alichomfanyia milliani na kumpelekea kupata ajali mbaya ambayo moja kwa moja yeye ndo muhusika Mkuu ,Alishindwa kuvumilia alijikuta akidondosha machozi mbele ya rafiki yake joas,Joas alitambua ni kwa nmna gni rafiki yake atakuwa anajisikia moyoni mwake ,ilibidi ampishe kwanza ili ampe Uhuru wa kutoa machozi ambayo yangepunguza uchungu na majuto makubwa moyoni mwake.
********** **************** 19
Anna alikuwa akijiandaa haraka haraka ili kwenda katika mkesha wa kuhitimisha bonanza la michezo lililokuwa likiendelea chuoni kwao,alivaa mavazi ya kupendeza ambayo yalizidi kumng'arisha sura yake nzuri na yakuvutia kwa mwanmme yoyote ambaye angemtazama .Moyoni mwake alikuwa na fumbo zito ambalo hakuna mwanamme yoyote ambae angeweza kulifumbua umbo hilo zaidi ya kijana mwenye asili kama yake ambae ni james,huyu ndo mvulana pekee ambae amefanikiwa kuuteka moyo wa msichana huyu kwa kiasi kikubwa tangu wakiwa utotoni,ukiachilia mbali hitaji la wazazi wa Anna na James kuwataka wao waoane,lakini pia Binti huyu alikuwa na mapenzi ya dhati kwa james.Alipomaliza kujiandaa alipanda taxi na kuelekea kwenye mkesha huo ,ambao Mara nyingi hushirikisha wanachuo wengi wenye uwezo na nguvu ya kifedha.
“Hellow miss ,hii”(habari mrembo,mambo)Ilikuwa ni sauti ya kijana mwenye asili ya kizungu,Gibson akimwambia Anna ,kijana mkorofi na anayetumia nguvu ya fedha katika kufanya vitu vingi ,”hii too”(mambo pia ),alijibu Anna huku akiinua grasi ya kinywaji ambacho alikuwa akikinywa taratibu akiendelea kufurahia wanasarakasi waliokuwa wakitumbuiza jukwaani, “can I join with you”(naweza kuungana na wewe?),aliuliza Gibson,huku akimuangalia msichana yule kwa macho yaliyojaa tamaa,”yeah ,you are wellcome”(ndio unakaribishwa)alijibu Anna huku akichezesha chezesha miguu yake.Gibson alikaa kwa muda huku akiwa anamuangalia binti huyo Mara kwa Mara kwa USO uliojaa matamanio .” Anna you are very beautifull”(Anna wewe ni mrembo sana)alivunja ukimya Gibson ,baada ya kuona ukimya umezidi kati yao.”thank you”(asante) alijibu Anna wa kujiamini ,huku akiangalia pembeni kukwepa USO wa Gibson ambao muda wote ulikuwa ukimuangalia.”I love you Anna”(nakupenda Anna)Aliongeza James na alijikuta akitamka maneno ambayo ndo yalimfanya aende alipokuwa binti yule mwenye asili ya kitanzania. “ok thank you but I already have fiance”(asante lakini ,tayari ninamchumba)alijibu Anna na kumkazia macho Gibson ambae kwa muda huo alikuwa amevurugika akilini kutokana na jibu hilo.”ok but take time to think about this , because I can’t let you go to another man”(sawa lakini chukua muda kufikiria hili kwa sababu swezi kukuacha uende kwa mwanamme mwingine)aliongea kwa kujiamini Gibson huku akionekana amepandwa na hasira,Anna alipoligundua hilo aliona Hamna haja ya kuendelea kuwa pale kwani maneno ya mwisho na ya hasira aliyoongea Gibson yalimfanya apate hofu moyoni mwake.Aliondoka taratibu eneo lile na kurudi nyumbani kupumzika .
************ ************”***
Taarifa iliyotolewa na askari wa barabarani waliokuwepo katika eneo ilipotokea ajali katika makutano ya barabara ya kutoka chuo cha northern Mariana university college,ajali ambayo ilihusisha magari madogo mawili ambapo gari moja lilikuwa ni la mwanachuo wa chuo hicho na mtoto Wa tajiri maarufu katika kisiwa hicho ,inaonesha chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa dereva wa gari ambayo ilikuwa inatokea chuo ,ambapo gari hiyo ilikuwa ikiendeshwa na millian ,ambaye kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na polisi ,binti huyu alikuwa anamawazo mengi hali iliyompelekea kuendesha gari bila kuwa na tahadhari na kujikuta akiingia kwa kasi katika barabara kuu na kusababisha ajali hiyo mbaya ambayo haikusababisha vifo lakini ilileta majeraha na madhara makubwa kwa madereva wote wawili waliokuwa ndani ya gari hizo. 20
Taarifa hii ilimfikia moja wa moja Mr Richard ambae bado kwa muda huo alikuwa nchini India akiendelea kumuuguza mtoto wake wa kike ambae japo madakitari walithibitisha kwamba hali yake inaendelea kuimarika siku hadi Siku lakini ilikuwa ni wiki ya nne sasa akiwa bado hajapata fahamu zake. Taarifa hii ilimshutua sana Mr Richard na alimuagiza msaidizi wake ambae alikuwa nchini Marekani katika visiwa vya Mariana ,kufuatilia chuoni na kupeleleza chanzo cha millian kuwa katika hali hiyo na kusababisha ajali ambayo ilitaka kuyagharimu maisha yake.
************* ***************
Anna aliamka asubuhi akiwa amechoka sana kutokana na kushinda akiwa katika mkesha çhuoni kwao,akiangalia watumbuizaji mbalimbali waliokuwa wakiendelea kutumbuiza katika mkesha huo wa kufunga tamasha la michezo lililokuwa likiendelea chuoni hapo.Alijivuta kitandani taratibu na kutupa shuka zito alililokuwa amejifunika usiku kucha kutokana na baridi Kali ambayo ilikuwepo siku hiyo katika jiji la new York .Alipokuwa akijiandaa kushusha miguu yake chini ili aende kufanya usafi wa mwili wake ,simu yake ya mkononi iliita ,ilijinyosha huku na huko na kisha kupiga miayo kadhaa ya kuondoa uchovu uliokuwa mwilini mwake,na akanyosha mkono kuchukua simu iliyokuwa pembeni ya kitanda chake na kuipokea .
“hallow”aliongea Anna akisubiri jibu la upande wa pili.
“Hallow Anna ,habari ya asubuhi?” ilikuwa nisauti ya mama yake na james,ambae ni mke wa Mr David.
“Salama mama shikamoo”aliamkia Anna huku akikaa kitandani vizuri.
“marhahaba ,inaonekana bado umelala eeh” aliuliza Mrs David,
“Hapana mama ndo nimeamka sasa hivi “alijibu Anna huku akitabasamu.
“Sawa nimeona umekuwa mkimya sana ,nikaona nikujulie hali mwanangu” aliongeza Mrs David.
“asante mama ,nilikuwa nimebanwa sana na masomo ila kesho nitakuja niwasalimie”alijitetea Anna.
“Vizuri nitafurahi ukija mwanangu ,maana Mimi mpweke sana sasa hivi na pia James ameniambia atakuja ndani ya siku tatu zijazo ”alisema Mrs David huku akicheka.
“aaha !! Kweli mama ? Sawa namsubiri nimuone maana ni Siku nyingi hatujaonana nae”aliongeza Anna huku akionyesha mapenzi ya wazi kwa james.
“sawa vizuri mwanangu ,wewe endelea na kazi zako tutaonana kesho”alimaliza Mrs david,
“Asante mama”alimaliza pia Anna nakukata simu .
Ni kweli usiopingika kwamba wazazi wa James walimpenda sana Anna tangu akiwa mdogo na ndio maana waliamua kuwaomba wazazi wa Anna ,kumuandaa Anna kuwa mke mtarajiwa wa james,na hili halikushindikana kutokana na urafiki wa karibu uliokuwepo tangu zamani baina ya familia hizi tajiri mbili,na hata Anna mwenyewe alionesha kumpenda sana James tangu wakiwa wadogo mpka sasa.
************ ************
Taarifa za chanzo cha ajali,ni mawazo aliyokuwa Nayo milliani yaliyosababisha yeye kupata ajali ,kwa uchunguzi uliofanywa na msaidizi wa mr richard katika chuo anachosoma milliani zinaonyesha msichana huyu alikuwa na ukaribu na kijana mwenye asili ya kiafrika anayeitwa 21
James,na hata siku aliyoondoka chuo kabla ya kupatwa na ajali,alikuwa akielekea kwa kijana kwa sababu zisizojulikana.Taarifa hizi zinamfikia mr Richard na anaagiza msaidizi wake amfatilie kijana huyu ili amfahamu na kisha atampa maagizo maalumu juu yake.