SAMAKI MTU(MERMAID)
SEHEMU YA SITA
Simulizi : SAMAKI MTU(MERMAID)
Mtunzi : Jackson James .
Mawasiliano; +255 762 892 472:, +255 652 064 958
Email: jamesjacson0@gmail.com
Taarifa za kutokea kwa ajali mbaya katika makutano ya barabara ilisambaa kwa haraka katika mitandao na vyombo mbalimbali vya habari,Taarifa hizi zilimfikia pia Mr Richard ambae ni baba mzazi wa milliani . Alikuwa yupo ofsini kwake akiendelea na shughuli zake za kila siku ,ndipo alipopokea simu kutoka hospitali alipokuwa amepelekwa binti yao kwaajili ya matibabu,Aliyempigia simu hiyo ni daktari Mkuu wa hospitali hiyo ambaye alimhitaji Mr Richard kufika hospitalini hapo haraka ,baada ya kupokea taarifa hizo akili yake ilizidiwa nguvu na mawazo mazito yaliyomjia 16
baada ya kusikia mtoto wake wa kutegemewa amepatwa na ajali mbaya ,alishindwa kujizuia na kujikuta akitoka nje ya ofisi yake kwa mwendo wa kasi ,kiasi cha kushitua wafanyakazi wake waliokuwa wakiendelea na shughuli zao za kawaida. Msaidizi wake ambae pia ni MTU anaeaminika sana kwa Mr Richard, pia aliziona taarifa zile kwenye televisheni iliyokuwa ikionyesha taarifa ya habari katika muda huo,alijua ni kwa namna gani Mkuu wake atakuwa anajisikia na hali atakayokuwa Nayo katika kipindi hicho.,Alitoka na kumfata bosi wake nje kwani alijua mahali atakapokuwa anaelekea si pengine Bali hospitalini,Alimuona Mr Richard nje ya gari lake akionekana kama ameishiwa nguvu na akiwa na mawazo mengi kichwani,Msaidizi yule anayeitwa Benson ,alijua fika kwa hali aliyonayo mr richard hataweza kuendesha gari,alisogea na kumuomba Mr Richard kama ataweza kumruhusu I’li ampeleke mahali anapohitaji kwenda. “Yeah you may drive, Thank you”(ndio unaweza kuendesha asante)alilibu Mr richard huku akijitahidi kufungua mlango wa gari yake kwa kasi lakini alisahau alikuwa ameufunga kwa namba maalumu,Alimuomba Benson amsaidie kufungua na wote wakapanda gari na kuanza safari ya kuelekea hospitalini.,safari nzima Mr Richard alikuwa ni MTU wa mawazo sana kiasi cha kusahau hata kumtaarifu mke wake juu ya jambo hilo la kushitua.
**************** *************
Katika hospitali ndogo ya genesis ndipo alipokuwa amelazwa James ,kutokana na kupoteza fahamu baada ya kupata mshtuko moyoni mwake,Aliempeleka hospitalini hapo ni rafiki yake wanayesoma nae darasa moja anayeitwa Joasi ,akishirikiana na wanachuo waliokuwa karibu katika eneo la tukio mahali alipoanguka James na kupoteza fahamu ,Ni katika hospitali hiyo hiyo alipolazwa Millian ambae yupo kwenye hali mbaya zaidi kwani amepoteza fahamu na amepata majeraha makubwa mwilini mwake ,hali ambayo inaonekana kukatisha tamaa watu wengi na madaktari pia.
Mr Richard alifika hospitalini hapo muda mfupi baada yakupokea taarifa lakini alishangaa kumuona mke wake akiwa ameshafika hospitalini hapo na alikuwa amekaa mahali pakupumzikia watu wanaofika kuona wagonjwa, Hali aliyokuwa Nayo mrs Richard ,ilikuwa ni Mara mbili au zaidi ya hali aliyokuwa nayo Mme wake,Kwani mama huyu wa kizungu alikuwa akibubujikwa machozi muda wote na alikuwa akianguka Mara kwa Mara kutokana na mshtuko mkubwa alioupata kutokana na kutotarajia kupata taarifa mbaya na za kushitua kama hizo katika muda huo. “am very sory my wife, its my own fault, that I failed to protect my daughter”(nisamehe sana mke wangu ni kosa language mwenyewe nimeshindwa kumlinda binti yangu)aliongea Mr Richard, kwa sauti ya huzuni huku machozi yakimtoka kama mtoto ,baada ya kumsogelea mke wake ambaye alikuwa amejiinamia akiwa katika dimbwi zito la mawazo, lakini alipogundua sauti ile ni ya Mme wake ,aliinuka na kumkumbatia Mme wake kwa nguvu huku,akilia kwa sauti kiasi cha kusababish watu waliokuwa karibu kubaki wakiwaangalia wazazi hao ambao walionekana wakipendana sana,hata Mr Benson, msaidizi Mkuu Mr Richard ,nae alishindwa kujizuia na kuanza kudondosha machozi. 17
Dakitari aliwaita wazazi wa millian ndani ya ofsi yake kwaajili ya mazungumzo juu ya hali aliyonayo binti yao kwa muda huo. “Doctor how is my daughter, is she fine?”(vipi hali ya binti yangu, dakitari ,ni mzima?)aliuliza kwa haraka mama yake na millian huku akijifuta machozi kwa kitaambaa chake alichokuwa ameshikilia mkononi. “yeah we thank god that we are doing all we can ,so that we can save her,because she is badly injured”_(ndio tunnashukuru mungu kwamba tunafanya kila tunaloweza Ili tuokoe maisha yake kwani ameumia vibaya”)_ alijibu dakitari huku akiwatazama kwa zamu wazazi wa millian waliokuwa wamezidi kuchanganyikiwa kutokana na taarifa hiyo. “doctor please help my daughter, “(dakitari Tafadhali msaidie binti yangu)aliongeza Mr Richard huku akiikamata mikono ya dakitari kwa nguvu. “We are doing our best sir”(tunajitahidi tuwezavyo Mzee)alijibu daktari huku akionesha wasiwasi usoni ,jambo ambalo Mr Richard aliligundua na alimuomba daktari kwenda kumuona binti yao,. Dakitari aliwaruhusu na alimuita mmoja wa wauguzi kuwapeleka chumba alichokuwemo millian,.walipofika kiukweli hawakuamini namna binti yao alivyoharibika mwili kutokana na majeraha makubwa yaliyokuwa yamekingwa na bandeji zilizokuwa zimezunguka kila sehemu,Alikuwa so millian waliyemzoea alikuwa ni MTU tofauti ambae hawakumtegemea kumkuta,Mama yake na millian alijikuta akiishiwa nguvu na kukaa chini ya kitanda cha mtoto wake,huku akijilazimisha asiamini kile alichokuwa akikiona mbele yake,Mr Richard alipoona Hall ya binti yake aliondoka kwa kasi chumbani mle na kuekekea kwenye chumba cha daktari ,alimuomba amuandikie ruhusa ya kumuamisha mtoto wake hosoitalini hapo Ili akapate matibabu zaidi nje ya nchi ya marekani,kwakuwa dakitari alikuwa akimfahamu vizuri Mr Richard, alikubali kumsaidia na aliomba apewe dakika kadhaa.Mr Richard alikubali na kutoka nje akamuendea Benson ,na kumtaka afatilie chanzo cha ajali hiyo na amletee ripoti Mara moja.
********** ***************
Mawimbi ya bahari yalipiga taratibu sana katika ukanda wa visiwa vya meriana asubuhi hiyo,kulikuwa na baridi kiasi iliyotakana na jua lililokuwa likiachia miale yake kwa mbali baada ya kuzidiwa nguvu na mawingu yaliyokuwa yamelizunguka katika kila hatua lilipokuwa likijaribu kusogea.
Pembeni ya ufukwe wa bahari katika mchanga laini anaonekana samaki mtu akiwa amejilaza,huku akiwa amejikunyata mikono yake kifuani huku miguu yake ambayo imeungana na kutengeneza mkia wa samaki mkubwa ,,ikiwa inacheza cheza katika maji ya bahari ambayo yalikuwa yanakupwa na kujaa hadi kiunoni kwake, Kwa mbali ukimuona kwa mbali samaki , huyu utadhani ni binti mrembo mwenye asili ya kizungu kutokana na umbile lake kuanzia kichwani hadi kiunoni kuwa sawa na binadamu wa kawaida , Kiumbe huyu siku ya leo alikuwa na mawazo mengi kichwani hasa akimuwaza binadamu aliyemsaidia wakati alipopatwa na tatizo wiki kadhaa zilizopita, Mwanzo yeye na samaki wenzake wa aina hii walikuwa wakiwaona binadamu kama viumbe wasiofaa na kuwaona kama maadaui zao ,lakini tangu asaidiwe na binadamu ,mtazamo wake juu ya binadamu ulibadilika na kuanza kuwaona kama viumbe wenye huruma,tofauti na alivyowaza mwanzo . Alitamani siku moja kijana yule aliyemsaidia aweze kurudi mahali pale walipokutana ili aweze kumuonesha shukrani zake kwa kuyaokoa maisha yake lakini 18
haikuwezekana kwani kijana yule hakuweza kurejea tena mahali hapo kwa muda wa wiki kadhaa sasa,japo samaki yule alijitahidi kuja mahali hapo kila siku lakini bado hakufanikiwa kumuona,moyoni mwake bado hakukata tamaa aliamini ipo siku atamuona,Alikaa kwa muda kisha akaamua kurudi makaoni kwake alipiga mbizi taratibu na kupotelea chini ya bahari.
**************** ****************
Asubuhi ya tarehe 25/6/2003 ,ndege ndogo ya kukodi ilikuwa ikipaa katika uwanja wa ndege wa Spain international airport kuelekea nchini india,ndani kukiwa na abiria wanne na rubani mmoja ,ambao ni Mr Richard na mke wake,pamoja na dakitari wa familia hiyo,wakiwa wanampeleka Millian ambae kwa muda wa siku kadhaa sasa tangu apate ajali hali yake si nzuri na hajapata fahamu na haikujulikana ni tatizo gani lililomkuta mwilini mwake kutokana na kutofanyiwa uchunguzi wa kutosha.